Kamati Kuu ya CCM Taifa Kukutana Leo

Nape Mnauye

KAMATI Kuu ya CCM Taifa itakutana Agosti 23, 2013 ikifuatiwa na Halmashauri Kuu keshokutwa asubuhi ambapo itakuwa kwa siku mbili.

Ajenda Kuu ya Kamati Kuu itakuwa kujadili maoni ya wana CCM juu ya rasimu ya Katiba, akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa White House, Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema mpaka sasa CCM na wanachama wake wameshirikiana vya kutosha kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Pia Kikao hicho kitajadili hali ya kisiasa na hatma ya madiwani Bukoba na Masuala Utumishi. Alisema siku ya Jumamosi asubuhi tarehe 24, kutakuwa na sherehe fupi za kuzindua Baraza la Ushauri la Wazee wa CCM kabla ya kikao cha halmashauri. Baraza hilo linaundwa na Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wastaafu wote wa CCM Taifa.