ILIKUWA ni majira ya saa 11.00 alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki, ambapo mtangazaji wa Radio VOA – Kiswahili, Sunday Shomari alisikika akimuhoji Kiongozi wa Ngoma Africa Band a.k.a FFU ughaibuni almaarufu “Watoto wa Mbwa” mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja mwenye makao kule Ujerumani.
Katika mahijiano hayo Shomari alikuwa anataka kujua haswa siri ya mafanikio ya Ngoma Africa band, na kwanini? bendi hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwateka washabiki wa kimataifa kwa kutumia muziki wa dansi. Kamanda Ras Makunja anakumbana na maswali ya asubuhi!
msikilize at http://www.voaswahili.com/audio/audio/177582.html