Ziara ya Waziri Kabaka ndani ya mabanda ya Wizara ya Fedha


Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuingia kwenye Banda la Wizara ya fedha kutembelea idara mbalimbali zilizo chini ya Wizara hiyo.


Waziri akianza safari ya kutembelea mabanda ya Wizara ya fedha, kushoto anaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Elizabeth Nyambibo.


Waziri Kabaka akitembelea banda la Mfuko wa Pensheni kwa Wafanyakazi wa Serikali (GEPF), Kulia ni baadhi ya wafanyakazi wa mfuko huo.


Waziri Kabaka akiwa ndani ya banda la PSPF akipata maelezo kuhusiana na nyumba za bei nafuu zinazojengwa na mfuko huo na kukopeshwa wanachama.


Waziri Kabaka akiwa ndani ya banda la Posta akitembelea shughuli anuai zinazoendeshwa na beki hiyo. Kulia anayetoa maelezo ni Ofisa Mwandamizi wa Benki ya Posta, Vicky Ngowi.


Hapa Naibu Katibu Mkuu Bi. Nyambibo akipata maelezo kutoka Mfuko wa Changamoto za Maendeleo ya Milenia (MCA-T), kulia ni Meneja Mawasiliano wa MCA-T, Margareth Mussai.
Picha zote na kitengo cha habari Wizara ya fedha.