Matukio Katika Warsha ya Wiki Moja kwa Redio za Jamii

Meneja wa mradi wa Amani na Demokrasi (DEP) kutoka UNESCO Courtney Ivins akizungumza na Mameneja na Wakurugenzi wa redio za jamii kupata tathmini ya warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa Juma wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

IMG_2735

Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO Yusuph Al-Amin asikiliza maoni wakati akiendesha mjadala wa namna ya ku-brand mradi wa Demokrasi na Amani (DEP) kuelekea uchaguzi 2015 kwa Mameneja na Wakurugenzi wa redio za jamii 25 nchini zilizohudhuria siku ya kufunga warsha ya wiki moja iliyoandaliwa na shirika la UNESCO na kufadhiliwa na UNDP.

IMG_2743

Washiriki wakijadiliana katika makundi mambo mbalimbali ya kuboresha kwenye redio jamii zao katika utekelezaji wa mradi wa DEP kuelekea uchaguzi 2015 wakati wa kuhitimisha warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa Juma.

IMG_2741

IMG_2739

Mkufunzi na Mshauri wa redio za jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu akifafanua jambo kwa Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO Yusuph Al-Amin wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja wa redio za jamii katika kuziandaa kuendesha mijadala ya Amani na Demokrasia kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.

IMG_2763

Msafiri Andrew kutoka Mpanda FM akiwasilisha maoni ya kikundi chake nini kifanyike katika utekelezaji wa mradi wa Demokrasia na Amani kwa redio za jamii kuelekea uchaguzi 2015.

IMG_2718

Meneja wa Triple A FM Borry Mbaraka akichangia maoni wakati wa kufunga warsha ya wiki moja kwa Wakurugenzi na Mameneja wa Redio za jamii nchini iliyomalizika mwishoni mwa wiki wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

IMG_2798

Meneja Mawasiliano wa Pangani FM Abdullah Mfuruki akichukua matukio mbalimbali ya kumbukumbu wakati wa kuhitimisha warsha warsha ya wiki moja iliyoandaliwa na UNESCO na kufadhiliwa na UNDP iliyowakutanisha Mameneja na Wakurugenzi wa radio za jamii 25 nchini kwa ajili ya kuwaandaa kuendesha mijadala ya Amani na Demokrasia kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.

IMG_2714

Sehemu ya washiriki ambao ni Mameneja na Wakurugenzi wa redio za jamii nchini waliohudhuria warsha hiyo ya wiki moja iliyomalizika mwishoni mwa Juma kwenye kituo cha Habari na Mawasiliano cha Telecentre wilayani Sengerema mkoani Mwanza iliyoandaliwa na shirika la UNESCO na kufadhiliwa na UNDP.

IMG_2813

Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Telecentre Sengerema FM mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye akitamka kufunga rasmi warsha ya wiki moja kwa redio za jamii katika kutekeleza mradi wa Demokrasia na Amani kuelekea uchaguzi 2015.

IMG_2823

Mshauri wa Redio za Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu akigana na Meneja wa Mradi wa DEP kutoka UNESCO Courtney Ivins mara baada ya kuhitimisha warsha ya wiki moja iliyokuwa ikifanyika kwenye kituo cha Habari na Mawasiliano cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza mwishoni Juma.

IMG_2825

Mameneja na Wakurugenzi wa redio za jamii nchini kwenye picha ya pamoja na wawezeshaji mara baada ya kumalizika kwa warsha ya wiki moja kwa ajili ya kuwaanda redio za jamii kuendesha mijadala ya Amani na Demokrasi kuelekea uchaguzi 2015 iliyoandaliwa na shirika la UNESCO na kufadhiliwa na UNDP.