FFU wa Ngoma Africa Band Watwaa Tena International Diaspora Award 2013

Kiongozi Mkuu wa Bendi ya Ngoma Afrika, Kamanda Rass Makunja akionesha tuzo walizotwaa.

Wasanii wa Ngoma Africa Band wakiwa na Tuzo ya kimataifa ya ‘Best Africa Band’

*Mabalozi wa Kiafrika nchini Ujerumani waipongeza

KWA mara nyingine tena Ngoma Africa Band aka FFU wamefanikiwa kutetea ubingwa wao wa Bendi Bora na kujichukulia tuzo ya kimataifa ya IDA mjini Tubingen, Ujerumani katika maonesho ya kimataifa ya International African Festival Tubingen 2013.

Bendi hiyo maarufu kwa kuwatia kiwewe mashabiki mdundiko wake imevunja rekodi kwa kuwa na washabiki wa kimataifa kila pembe. Katika maonesho ya International African Festival 2013, yaliyofanyika mjini Tubingen, Ujerumani Ngoma Africa Band imekubalika na washabiki hivyo kutwaa tuzo hiyo. FFU sasa si kwamba inakubalika kwa wapenzi wake tu bali pia kwa mabalozi kutoka nchi mbalimbali za kiafrika nchini Ujerumani.

Tusikose kuwasikiliza ffu at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com