Kampuni ya Bia ya SBL Yazinduwa Muonekano Mpya wa Kibo Gold

Meneja wa Miradi Endelevu na Uwajibikaji, Nandi Mwiyombella akizungumza

Kampuni ya Bia ya SBL Yazinduwa Muonekano Mpya wa Kibo Gold

*Sasa Kibo yang’ara katika chupa ya kisasa kabisa

KAMPUNI ya bia ya Serengeti leo imezindua muonekano mpya wa bia inayosherehekewa sana mkoani hapa, Kibo Gold. Uzinduzi huu uliofanyika katika kiwanda cha bia cha Serengeti kilichopo Moshi, ulifikia kileleni kwa shughuli murua iliyoandaliwa na kampuni hii na kushuhudiwa na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali. Bia hii ya Kibo sasa inamuonekano mpya wa chupa inayoashiria ubora wa kilichopo ndani. Bia ni yenye ubora uleule wenye kiwango cha hali ya juu ila kwa chupa ya rangi ileile iliyong’arishwa na shingo ndefu.

Akiongea kwenye hafla hii Meneja wa miradi endelevu na uwajibikaji, Nandi Mwiyombella alisema bia hii ya Kibo Gold imekuwa ikitambulika kwa ubora na ladha nzuri kwa wateja.
“Kwa muonekano huu mpya wa chupa ya kisasa, tunaamini wateja wengi watavutiwa na kuipenda zaidi kwanini muonekano unaokwenda na wakati.
Ubora wa bia hii, inakuwa dhahiri kweli kabisa ukizingatia kwamba inatengenezwa kwa maji yatiririkayo kutoka katika kilele cha juu kabisa cha Mlima Kilimanjaro ambapo pia bia inazoa jina lake hili la ‘KIBO’, “ aliongeza Bi Nandi.
Kampuni ya bia Serengeti chini ya kampuni mama ya Diageo, inazingatia kanuni na sheria zilizowekwa na kampuni hii kwenye ubora katika uzalishaji wa bidhaa zote. Muonekano wa bidhaa ni uleunaondena na soko za kimataifa na wa kuvutia. Kampuni ya bia ya Serengeti inatumia malighafi za kitanzania ili kuleta ubora halisi na vile vile kukuza uchumi wa Tanzania katika sekta ya kilimo.
Kwa Mhariri: Bia ya Kibo Gold ilirudishwa sokoni hapa Tanzania mwaka jana, 2012, mwezi wa sita baada ya kuwa haipo kwenye soko kadri ya miaka kumi. Ni mojawapo ya bia zinazoongoza nyanda za kaskazini sasa hivi. Bia hii inazalishwa katika kiwanda cha bia cha Serengeti cha Moshi nainasambazwa mkoani hapo na mikoa jirani, Arusha, Tanga, ManyaranaTangakwawingi.

Kampuni ya Bia ya SBL Yazinduwa Muonekano Mpya wa Kibo Gold

Tafadhali kunywa kistaarabu. Haiuzwi kwa waliochini ya miaka 18.