Mambo ya kuzingatiwa na Kamati za Bunge katika kusimamia fedha naRasilimali za UmmaZitto Kabwe
Utangulizi
Katika madaraka yote ambayo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaimetoa kwa Bunge kwa mujibu wa ibara ya 63, wajibu wa ‘kuisimamia Serikali’ndio wajibu unaoelezea hasa kazi za Kamati za Bunge. Ni kupitia Kamati zaBunge, za kisekta au za mahesabu, Serikali huwajibika kujieleza kinaga ubagakuhusu mipango yake,kuomba fedha na kuelezea matumizi ya Fedha hizo.Mfumo wa utendaji kazi wa Kamati za Bunge ni mfumo ambao unawezakuimarisha uwajibikaji nchini na hivyo rasilimali za nchi kutumika vema nakuendeleza wananchi.
Mfumo dhaifu wa Kamati za Bunge huipa fursa Serikalikufanya itakavyo na kuimarisha ufisadi kama vile matumizi matumizi mabaya yamadaraka, wizi, udanganyifu,hongo,uzembe uvivu.Mada hii itajikita katika maeneo ya kuzingatia ili kuwezesha Kamati za Bungekusimamia misingi ya Uwajibikaji na hivyo kuzuia ufisadi na kuelekeza rasilimali zanchi kwenye maeneo ya Maendeleo ya wananchi badala ya anasa nakutajirisha kundi dogo la viongozi.Tutaona majukumu ya Kamati katikakusimamia Fedha za Umma na maeneo muhimu sana ya kuweka kipaumbelekatika usimamizi huo. Tutaona changamoto za Kamati na namna ya kuzitatua ilikuwezesha Bunge kutekeleza wajibu wake inavyopasa.
UWAJIBIKAJI
Demokrasia ya kibunge ni moja ya mfumo wa kutazamana kati ya Tawi laUtendaji (tunaita Serikali), Tawi la Uwakilishi (Bunge) na Tawi la utekelezaji waSheria (mahakama). Demokrasia inajumuisha uwajibikaji katika matumizi yamadaraka (McGee, D 2002). Uwajibikaji ni pamoja na kuweka mifumo yakuwezesha maamuzi kufanyika kwa namna ambayo uadilifu unazingatiwa nakwa ufanisi. Uwajibikaji unapaswa kuhusisha matawi yote ya Serikali na jamii kwakupitia asasi za kiraia na vyombo vya habari.Ibara ya 63 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imegawamadaraka kwa Mhimili wa Bunge ambapo majukumu matatu makuuyameainishwa, nayo ni Uwakilishi, Kuisimamia Serikali na Kutunga sheria.
Kwakupitia mambo kama kuuliza maswali kwa mawaziri na maswali ya papo kwapapo kwa Waziri Mkuu, kuwasilisha hoja binafsi, kuwasilisha miswada binafsi nakujadili miswada ya Serikali, hoja ya kuahirisha Bunge nk, Bunge huwezakuifanya Serikali kuwajibika kwayo. Kamati za Bunge mahesabu – Kamati yaHesabu za Serikali, Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaana Kamati ya Bajeti, nimuundombinu muhimu sana katika kuhakikisha kuwa Serikali inajieleza na kujibu
hoja kuhusu sera zake na namna inavyotekeleza sera hizo, maombi ya fedha namatumizi ya fedha hizo ili kufanikisha sera za Serikali.Uwajibikaji hauna lengo tu la kukamata watu wanaovunja sheria bali unalengola kuweka mfumo ambapo kila mtu mwenye mamlaka anajibu kwa matendoyake na hata pale asipotenda ikiwa alitakiwa kutenda (answerable to actionsand inactions).
Uwajibikaji unajenga tabia ya watu, na hasa watu wenyemamlaka, kuzingatia Katiba, Sheria, kanuni na taratibu katika kufikia maamuziyao.Iwapo mtu mwenye mamlaka akifanya jambo ambalo hawezi kulitetea mbeleya umma, au analionea aibu kulielezea, ni dalili kubwa kwamba jambo hilo auuamuzi huo unatokana na rushwa. Uwajibikaji unaweza mfumo ambao kila mtumwenye mamlaka atapaswa kujielezea na kutetea uamuzi wake hadharani.Kwa mfano, Waziri anapochukua uamuzi fulani wa kisera akijua kuwa ni lazimauamuzi ule aujibie maswali ndani ya Bunge, itamfanya Waziri huyo afanyeuamuzi mzuri na wenye maslahi kwa Taifa. Lakini kama Waziri huyo anaweza‘kuwaona’ wabunge fulani na kuwataka wamlinde kwa uamuzi huo ni dhahiriuamuzi huo ni wa kutilia mashaka maana jambo jema halihitaji kulindwa. Hivyowakati mwingine uwajibikaji huonekana kufanyika ilhali ufanisi haupo kwanisehemu fulani ya Wabunge inakuwa imeamua kutetea jambo lolote linaloletwana Waziri aliyezungumza kabla na wabunge.
Hii ndio hatari kubwa sanainayokabili mabunge mengi duniani.Wakati kila mwaka Kamati ya Bajeti inapaswa kusimamia uwajibikaji katikamapato ya Serikali (finance bill) na mgawanyo wake (appropriation bill), Kamatiza Mahesabu zina wajibu wa kutumia sheria hizo kuhakikisha (i) makusanyo yafedha hizo yamekusanywa kama ilivyoombwa na kuidhinishwa na Bunge na (ii)Matumizi ya Fedha hizo yamefanyika kama ilivyoidhinishwa na kwa kuzingatiathamani ya fedha (value for money).
KAMATI ZA BUNGE ZA MAHESABU
Kamati za Bunge za Mahesabu ni asasi muhimu za Bunge katika kuhakikishaSerikali inawajibika kwa wawakilishi wa wananchi. Majukumu ya kamati hiziyameainishwa na Kanuni za Bunge, nyongeza ya nane. Kama tutakavyoonakatika kiambatanisho cha mada hii, majukumu yote yanahusisha kaziiliyofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Nyarakamuhimu na ya kwanza katika kazi za Kamati za kusimamia mahesabu ni Ripotiya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Hivyo Kamati za Bunge zamahesabu na CAG wanapaswa kufanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikianomkubwa sana. Ndio maana Bajeti ya CAG inapitishwa na Kamati ya PAC naikishapitishwa hakuna mamlaka ya kuhoji tena. Vile vile PAC ndio Kamati yenyemamlaka ya kuteua Mkaguzi wa kukagua mahesabu ya Ofisi ya CAG.
Ni wajibu wa Kamati za Bunge za mahesabu kulisaidia Bunge katika kuiwajibishaSerikali. Mara kadhaa kumekuwa na maelezo kwamba kazi ya Bunge nikuishauri Serikali, hapana. Katika kuisimamia Serikali ndani yake kuna kunaushauri hivyo ushauri haupaswi kuwekewa mkazo zaidi ya usimamizi. Warasimuwa Serikali wanapenda neno ushauri na kuchukia neno usimamizi. Wabungehawapaswi kuingia katika mtego wa ‘kazi yao ni kushauri’ kwani huo ni mtegouliotegwa na warasimu ili kupunguza nguvu ya Bunge. Kazi ya Bunge nikusimamia Serikali.
Kamati za Bunge za mahesabu ndio zenye kubeba mzigohuo mkubwa sana kwa niaba ya Bunge.Hivyo tutaona ni namna gani uadilifu ni jambo la msingi sana katika wajibu huu. Vilevile ndio maana ni rahisi sana kuonaKamati za Mahesabu zikipewa kila aina ya shutuma kutoka kwa wasimamiwana wakati mwingine kwa kuwatumia baadhi ya Wabunge kwa kujua aukutokujua.Wakati mwingine Kamati za Bunge huambiwa kuangalia ‘mahesabu tu’ basi. Niwajibu wa Kamati za Bunge kuangalia mahesabu ya Umma na kuona kamamatumizi ya Fedha za Umma yanafanikisha malengo yaliyotarajiwa(performance audit). Itakuwa ni uwendawazimu kwa Kamati kuridhika kwakuangalia tu mizania ya Serikali au Mashirika ya Umma au Serikali za Mitaa. Kwamfano ni wajibu wa Kamati kuangalia kama Fedha zilizotolewa kwa ujenzi waBarabara zimetumika kwa kazi hiyo.
Ni wajibu zaidi wa kamati kuangalia kamagharama hiyo iliyotumika kujenga barabara husika ndio gharama halisi na siokwamba imezidishwa ili kunufaisha watu wachache. Ni wajibu mkubwa zaidi wakamati kaungalia kama barabara hiyo imejengwa kwa kiwango kinachotakiwa.Hii inaitwa ‘value for money’.Katika utendaji wa Kazi hizi ni muhimu na lazima, Kamati za Bunge kutumiakwanza Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Hata hivyoKamati pia zaweza kutumia taarifa kutoka vyanzo vingine mbalimbali kamawananchi na vyombo vya habari katika kufikia malengo ya kuchunguza. Kwamfano, hivi karibuni moja ya Magazeti hapa nchini (Gazeti la Jamhuri) liliandikakuhusu matumizi mabaya ya fedha katika Mkutano wa Smart Partnership. Kwamba takribani shilingi bilioni nane zimefanyiwa ufisadi.
Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali amenukuliwa akisema kwamba hajapat baruayeyote inayomwomba (CAG haagizwi, anaombwa) kufanya ukaguzi maalumuwa mkutano ule. Kamati ya Bunge ya PAC inaweza kutumia mamlaka yakekumwomba CAG kufanya ukaguzi maalumu na kuwasilisha matokeo yakekwenye Kamati na hatimaye Bungeni. Iliyokuwa Kamati ya POAC ilifanya wajibuhuu vizuri sana kwenye suala la nyumba ya Gavana wa Benki Kuu na kutokanana ukaguzi huo hoja ile ilifungwa.Ili kutekeleza wajibu huu muhimu wa uwajibikaji, Kamati za Bunge za mahesabuni lazima ziwezeshwe vya kutosha kwa mafunzo ya ujuzi (skills) na maarifa (knowledge).
Bila ya kuwa na uelewa mpana wa mambo Kamati hujikutazikifanya maamuzi ambayo yanakuwa na madhara makubwa kwa Taifa.Katika kutekeleza wajibu, ni muhimu na lazima wajumbe wa Kamati kujiepushana vitendo vya rushwa kwani vitendo hivyo huzuia usimamizi na hatimayekuendeleza rushwa kwa wanaosimamiwa. Uwajibikaji ni silaha dhidi ya rushwana hivyo wanaosimaima uwajibikaji ni lazima wawe wasafi wao binafsi kwanzakabla ya kusafisha walio wachafu. Uadilifu ni msingi muhimu sana katikakujenga uwajibikaji. Bila ya uadilifu hakuna uwajibikaji na vile vile kukosekanakwa uwajibikaji humomonyoa utamaduni wa uadilifu katika jamii.
Mambo gani ya kuzingatia?
Tumeona Wajibu wa Kamati katika kusimamia uwajibikaji wa Serikali.Kiambatanisho kimeweka kinabaga ubaga majukumu na wajibu huo. Masualamachache yafuatayo ni ya kuzingatia sana katika utekelezaji wa wajibu huu.
Moja
Pamoja na Matumizi yote ya Serikali ambayo Kamati husimamia,kunamatumizi ambayo inabidi kuweka msisitizo maalumu. Moja ya matumizi hayo niya Deni la Taifa. Katika Ripoti ya CAG ya mwaka 2012, hoja za kuhusu Deni laTaifa zimeendelea kutokana na kasi ya ongezeko la Deni. Kamati inapaswakufahamu kwamba Mzigo mkubwa wa Deni la Taifa ni katika kulipa ambapoFedha nyingi za umma hutumika. Kila mwaka Bajeti ya kuhudumia Deni la Taifahuwa ni moja ya Bajeti kubwa zaidi ya Bajeti nyingine zote. Kwa mfano mwaka2012/13, Serikali ilitenga takribani shilingi trilioni mbili kuhudumia Deni laTaifapeke yake ilhali robo tu ya fedha hizo ilitengwa kwa ajili ya Wizara ya Afya.Kamati zinapaswa kukagua kwa kina na kila wakati matumizi ya mikopo ilikuhakikisha kwamba mikopo mingi inatumika kujenga uwezo wa nchi kuzalisharasilimali za kuhudumia mikopo hiyo kwa kukuza uchumi, kuzalisha ajira nakuongeza kodi.
Pili
Makusanyo ya Kodi ya Serikali. Bunge hupitisha fedha kuwezesha Mamlakaya Mapato Tanzania kukusanya kodi. Hivi sasa ni takribani Watanzania milionimoja tu ndio wanalipa kodi (kwa maana ya watu binafsi walio kwenye mfumorasmi). Hivyo tuna wigo mdogo sana wa kodi wakati tunatumia fedha nyingisana kukusanya kodi hiyo kidogo. Ni Wajibu wa Kamati kuona kwamba ufanisikatika kukusanya kodi unafikiwa ikiwemo kwa kiasi kikubwa sana kuzuia mianyaya ukwepaji wa kodi. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, asilimia 15 ya makusanyotarajiwa huwa hayakusanywi kwenye idara ya Mapato peke yake kutokana naukwepaji wa Kodi. Hii ni sawa na takribani shilingi 490 bilioni kwa kutumiamakadirio ya mwaka wa fedha 2012/13. Wakati Bandari ya Dar es Salaam inapakua makontena 600 kwa siku, kuna wakala wa upakuaji (clearingandforwarding agents) wa idadi hiyo hiyo katika Bandari hiyo. Haiwezekani kuwe nawastani wa kontena moja kwa kila wakala. Eneo hili linahitaji jicho pevu kutoka
kwenye Kamati za Bunge na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.Ukwepaji kodi wa makampuni ya kimataifa pia ni ajenda kubwa ambayo kilamara kamati inapaswa kuizingatia ili kuzuia.Kamati ya PAC tayari imepitisha pendekezo la ukaguzi wa misamaha ya kodina kuiweka wazi (audit of tax exemptions and transparency). Ni matarajiokwamba kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwamwaka unaoishia Juni 2013 Watanzania wataona taarfa ya ukaguzi wamisamaha ya kodi.
Tatu
ukaguzi wa mikataba na taratibu za Manunuzi.
Hili ni eneo ambalolimekuwa chanzo kikubwa cha ubadhirifu katika nchi yetu. Ni muhimu kila marakamati kuzinagtia eneo hili katika kazi zake. Eneo hili linaathiri zaidi Mamlaka zaSerikali za Mitaa ambapo udokozi imekuwa kama utamaduni na hivyokuzorotesha utoaji wa huduma kwa wananchi. Ni muhimu Kamati kuhitaji marakwa mara ukaguzi maalumu kwenye manunuzi ili kujenga uwajibikaji katikaeneo hilo na kuepusha hasara kubwa kwa nchi.
Nne
hivi sasa nchi yetu imekuwa kitovu cha biashara ya dawa za kulevya.
Vijana wa kitanzania wamekuwa wakikamatwa maeneo mbalimbali dunianiwakihusishwa na biashara ya madawa ya kulevya. Moja ya njia ya kupambanana uharamia huu ni uwajibikaji wa mamlaka zenye wajibu wa kupambana namadawa ya kulevya. Hivyo, Kamati za Bunge zihoji katika mahesabu yamamlaka hizo matumizi ya fedha za umma kupambana na biashara yamadawa ya kulevya ilhali biashara hiyo inazidi kushamiri. Iwapo tutawajibishaWizara ya mambo ya ndani kitengo cha kupambana na madawa ya kulevyatutakuwa tumechangia katika vita hii. Hatuwezi kuwa tunatenga fedha kilamwaka dhidi ya biashara hii haramu lakini bado inazidi kushamiri. Kila mwenyewajibu awajibishwe.
Mwisho
Ukaguzi wa zoezi la ubinafsishaji.
Bado sera ya ubinafshishajiinatekelezwa na Serikali. Ni wajibu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali kukagua zoezi la ubinafsishaji na Kamati za Bunge kusimamia uwajibikajikatika zoezi hili. Ubinafsishaji ni uuzaji wa mali ya Umma, hivyo ni lazima upateusimamizi kamilifu.
Hitimisho
Kamati za Bunge za Mahesabu ni asasi muhimu za demokrasia kwani husimamiauwajibikaji. Ni vema kamati hizi kupewa uzito stahili kwa kuwa na rasilimali zakutosha katika kufanya kazi zake na kuhakikisha taarifa zake zinapata uzitokatika utekelezaji. Kimsingi Kamati zote za Bunge ni sawa kihadhi lakini Kamati zamahesabu ndio Bunge kiuhalisia.