Waziri Mkuu Thailand, Shinwatra Amaliza Ziara Tanzania

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinwatra wakati wa kuondoka kurejea nyumbani kwa mgeni wake huyo baada ya kuhitimisha kwa mafanikio makubwa ziara rasmi ya siku tatu hapa nchini Agosti 1, 2013.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinwatra wakati wa kuondoka kurejea nyumbani kwa mgeni wake huyo baada ya kuhitimisha kwa mafanikio makubwa ziara rasmi ya siku tatu hapa nchini Agosti 1, 2013.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akiwa na baadhi ya viongozi wa jiji la Dar es salaam wakipunga mkono kumuaga rasmi Waziri mkuu wa Thailand katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere. Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.

Wasanii wakishangilia wakati ndege iliyomchukua Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinwatra ikipaa wakati wa kuondoka kurejea nyumbani kwa mgeni huyo baada ya kuhitimisha kwa mafanikio makubwa ziara rasmi ya siku tatu hapa nchini Agosti 1, 2013.

Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kushoto) akiwasili uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara akiwa ameambatana na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete (katikati). Bi. Shinawatra amemaliza ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania. 

Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinwatra akipeana mikono na viongozi anuai wakati wa kuondoka kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha kwa mafanikio makubwa ziara rasmi ya siku tatu hapa nchini Agosti 1, 2013. (Picha zote na IKULU na Habari Maelezo)