Picha mbalimbali ndani ya manesho ya Saba Saba


Wananchi wakiangalia mfano wa viungo mbalimbali vya mwili wa binadamu na kupewa maelezo ya namna vinavyofanya kazi mwilini, ndani ya banda la Moi kwenye maonesho ya 35 ya Biashara Kimataifa


Umati wananchi waliotembelea maonesho ya Saba Saba ndani ya viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere wakiwa wamemzunguka Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete alipotembelea maonesho hayo Julai 6, 2011.


Pichani kulia ni baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wakitoa maelezo kwa mmoja wa wateja waliotembelea banda hilo ndani ya Maonesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa viwanja vya Saba Saba jijini Dar es Salaam.