Rais Jakaya Kikwete akitawazwa kuwa OMUKAMA wa Missenyi wakati wa
ziara yake ya siku sita mkoani Kagera. Anayemsimika ni kiongozi wa wazee wa Missenyi, Mzee Ernest Babeiya.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelefu ya wananchi wa mkoa wa Kagera
waliofurika katika uwanja wa michezo wa Kaitaba kumsikiliza siku ya mwisho ya ziara yake ya siku sita mkoani humo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelefu ya wananchi wa mkoa wa Kagera waliofurika katika uwanja wa michezo wa Kaitaba kumsikiliza siku ya mwisho ya ziara yake ya siku sita mkoani humo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kyaka-Bugene kwa kiwango cha lami katika kijiji cha Bunazi, mkoani Kagera, akiwa na mawaziri
alioongozana nao katika ziara yake hiyo ya siku sita mkoani humo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kyaka-Bugene kwa kiwango cha lami katika kijiji cha Bunazi, mkoani Kagera, akiwa na mawaziri alioongozana nao katika ziara yake hiyo ya siku sita mkoani humo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wanahabari wa vyombo
mbalimbali wa mkoa wa Kagera ambao waliongozana naye katika ziara yake ya siku sita mkoani
humo. Rais Kikwete amewapongeza wanahabari hao na kutoa shukurani nyingi kwa kazi nzuri ya
kuufahamisha umma kila hatua ya ziara yake kwa ufasaha na weledi. Wanahabari hao pia wamefurahi kuona kwamba Rais hakuja na jopo la wanahabari kutoka Dar es Salaam kwa kuwaamini wao, hatua anbayo wamesema imewapa faraja na furaha kubwa na kujiamini zaidi. PICHA NA IKULU