UMOJA wa Watanzania Nchini Ujerumani (UTU) kwa kasi kubwa unaendelea kupeperusha vema bendera ya Tanzania huko Ughaibuni kwa kutumia nafasi zote wanazopewa nchi Ujerumani.
Hivi karibuni Umoja huo ulishiriki katika maonesho ya “Brüderschaft der völker” mjini Aschaffenburg na kutangaza vema tamaduni za nchi yetu, ambapo katika onesho hilo wageni wengi walivutiwa na shughuli za Umoja huo za kuitangaza Tanzania.
Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) unatilia mkazo katika suala zima la kuwashawishi wadau wa
kimataifa kuwekeza katika huduma anuai nchini Tanzania hasa za kijamii kama vile Elimu, Afya n.k.
Umoja huo umepokea mialiko ya kushiriki maonyesho mengine yakiwemo makubwa kama International African Festival Tubingen 2013 yatakayo anza 8 hadi 11.08.2013
usikose kuwasiliana nao kupitia:kamati.utu@googlemail.com