Mwaliko kwa Wadau wa Elimu na Katiba Tanzania

TGNP bango linaloonesha ofisi za TGNP


 
RE: MWALIKO KUHUDHURIA NA KUSHIRIKI SEMINA MAALUMU YA WAZI YA KIJAMII KUHUSU KATIBA MPYA NA ANGUKO LA ELIMU NCHINI YA TAREHE 31 JULAI, 2013 VIWANJA VYA MTANDAO WA JINSIA (TGNP) MABIBO
 
Salaam kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)!
 
Rejea kichwa cha habari hapo juu. Mtandao wa Jinsia Tanzania tunapenda kuwaalika wadau wa elimu na katiba mpya kuja kuhudhuria na kushiriki semina ya wazi ya kijamii(GDSS) pia kuungana na wadau wa elimu wengine ili kwa pamoja tushiriki semina maalamu, tujadili kwa pamoja na tutoe maoni yetu kwa malengo ya kuokoa hali ya elimu nchini na hatima ya kizazi kijacho. Mada katika semina hii itakuwa; ‘Katiba Mpya na Anguko la Elimu Nchini’. Itafanyika Mabibo, maeneo ya viwanja vya TGNP, itakuwa siku ya Juma Tano tarehe 31/7/2013, semina itaaanza saa 9 mchana na itamalizika saa 11 jioni, mtoa mada ni Fausta Musokwa kutoka HakiElimu.  
 
Tunawaomba pia msambaze ujumbe kwa wadau wengine wengi ili wahudhurie kwa wingi na kilio cha wengi kisikike kwa watunga sera ya huduma ya elimu kwa ajili ya kuliokoa taifa letu. Mada hii imeandaliwa baada ya kufuatilia mwenendo wa matokeo ya mitihani ya kitaifa kuanzia ngazi ya shule za msingi mpaka shule za sekodari ulioonesha udororaji endelevu wa elimu nchini tangu mwaka 2009 mpaka sasa.
 
Katika semina hizi (GDSS) ambazo hufanyika mara moja kwa wiki kila siku ya Juma Tano, washiriki hupashana habari mbalimbali, hujengeana uwezo, hujifunza, na kujenga mtandao wa nguvu za ukombozi na kuleta mabadiliko katika jamii.
 
Ushiriki wenu utawezesha mafanikio ya semina hiyo.
  
Wenu katika juhudi za kuleta mabadiliko endelevu katika sekta ya elimu.

Demetria Kalogosho
Mratibu wa semina za jinsia, TGNP