MWANAMUME anayetuhumiwa kwa makosa mengi ya umbakaji, ‘mbakaji sugu’ nchini Afrika Kusini, Sifiso Makhubo, amekutwa akiwa amefariki katika chumba chake gerezani.
Sifiso Makhubo, aliyekuwa anakabiliwa na mashtaka 122 yakiwemo ya mauaji na ubakaji amekutwa akiwa amekufa huku ikiaminika amejinyonga kwa kutumia blanketi alilokuwa nalo katika chumba chake.
Baadhi ya makosa aliyoshtakiwa nayo Makhubo ni pamoja na kuwaambukiza virusi vya HIV watu aliojamiiana nao kwa makusudi. Afrika Kusini ina ina matukio mengi zaidi ya ubakaji duniani, huku takwimu za Polisi zikionesha kuwa ni matukio 64,000 pekee ya ubakaji ndio yalioripotiwa kwa mwaka 2012 tu.
Maofisa wa polisi wanasema Makhubo alikuwa peke yake katika chumba cha selo yake alichokuwa, hata hivyo uchunguzi unafanywa ili kujua nini kilisababisa tukio hilo la yeye kujinyonga.
Mtuhumiwa Makhubo anatuhumiwa kwa kuwabaka watoto 35 na wanawake wawili, kati ya mwezi Januari mwaka 2006 na Februari 2011. Hadi sasa uchunguzi uliofanywa wa DNA katika walalamikaji waliobakwa ulibaini kuwa yeye ndiye alikuwa mbakaji.
-BBC