IMEBAINIKA kuwa balozi za nchi za Ulaya zilizopo nchini Tanzania, zikiwemo
balozi za Ujerumani, Ubelgiji, Netherland na nyinginezo zimekuwa zikiweka vikwazo kwa baadhi ya raia wa Tanzania wanaohitaji pasi za kusafaria kwenda katika nchi za ulaya.
Taarifa zinasema licha ya baadhi ya Watanzania kutimiza masharti yote yanayohitajika katika kuomba pasi, lakini balozi hizo zimekuwa zikiwawekea vikwazo visivyo katika sheria za maombi ya pasi. “…Mfano Mtanzania anapo omba pasi ya ubalozini atapeleka barua ya mwaliko na bima, pamoja na taarifa ya benki (benk statment), barua ya kazini, nakala za mishahara. Heti bado maofisa balozi wanadai barua nyingine itoke kwa mwenyeji kuonesha uhusiano na mgeni Mtanzania! Kwa kweli hakuna uhusiano mzuri katika ya raia na maofisa wa visa wa balozi za EU nchini Tanzania,” kilieleza chanzo.
“…Kimsingi Watanzania wanapoomba pasi za Ulaya wanasumbuliwa sana hapa nchini. Serikali inaweza kuwa na uhusiano mzuri na balozi hizo lakini raia wa Tanzania hawathaminiwi kabisa na balozi za EU hapa Tanzania,” kilieleza chanzo.