RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete Julai 18, 2013, alikutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi – CUF, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, viongozi hao wawili wamezungumzia masuala ya kitaifa na jinsi gani wadau mbali mbali wanavyoweza kuendelea kushirikiana katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Tanzania.