Mbunge Beatrice Shellukindo, Meya Silaa Watembelea Banda la APRM, Sabasaba

Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutemnelea Banda la Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) kwenye Maonesho ya Saba Saba juzi (Jumatano). Kulia ni Ofisa wa APRM Tanzania Bi, Praxida Gasper.

Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwa katika picha na wafanyakazi wa APRM na AICC mara baada ya kutembelea banda zilizomo taasisi hizo.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano katika Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM), Bw. Hassan Abbas akimpa maelekezo juu ya kazi za APRM mmoja wa raia wa kigeni aliyejitambulisha kuwa ni raia wa Marekani kwenye maonesho ya Sabasaba. (Picha zote kwa hisani ya APRM Tanzania)