Muonekano wa Banda la MeTL Group lililopo kwenye maonyesho ya 37 kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwa na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji wakati alipotembelea Banda la Kampuni hiyo kwenye maonyesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Bw. Hussein Dewji ambapo pia alimpongeza kwa bidhaa nzuri wanazozalisha katika kampuni yao.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akisalimiana na warembo wanaotoa huduma katika banda hilo ambao wamevalia Khanga zinazotengenezwa kiwanda cha 21 Century Textile cha MeTL .
Pichani juu na Chini ni Wananchi wakimiminika kwenye Banda la kampuni ya MeTL Group kujipatia mahitaji mbalimbali ya nyumbani zikiwemo Sabuni za kufulia, Unga, Mafuta ya kupikia, Vitenge, Khanga na vingine vingi.
Baadhi ya Kinamama wakisaidiwa kuchagua Khanga na Vitenge na mmoja wa warembo nadhifu wa MeTL wanaotoa huduma kwa wateja katika banda hilo.
Bidhaa mpya ya Kampuni ya MeTL Group “Sheeba Shake” yenye ladha tatu za kuvutia ikiwemo Vanilla, Chocolate na Banana. Kinywaji hicho kitaingia mtaani baada ya maonesho haya kumalizika. Kinatia nguvu na kukuburudisha.