Ofisa Tawala Mwandamizi Bw. E. Ndofi kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali Wizara ya Fedha, akitoa ufafanuzi kuhusu watumishi wa Idara na Vitengo vilivyopo kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali wakati wa maonesho ya wiki ya utumishi wa umma Nchini Ghana.
Msemaji wa Wizara ya Fedha akiwa ameambatana na washiriki wengine kutoka wizara ya fedha wakiwa kwenye banda la Zimbambwe wakibadilishana uzoefu juu ya utendaji kazi katika nyanja mbalimbali walipokuwa Nchini Ghana.
Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Mikataba Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Steven H. Issack alipotembelea banda la wizara ya fedha kutaka kupata ufafanuzi juu ya uanzishwaji wa mikopo kwa watumishi wa umma kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali, kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Bi. Christine Ngonyani na kulia ni Bi. Miriam Mnzava Nchini Ghana.
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa Wizara ya Fedha kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bi. Christine akiwaeleza wananchi wa Ghana jinsi idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali inavyosaidia Watumishi wa Umma katika kupata Mikopo.
Washiriki kutoka Nchi mbalimbali walipotembelea katika makumbusho ya taifa ya Ghana.
Washiriki wa Maonesho ya Wiki ya Utumishiwa Umma kutoka Tanzania na nchi nyingine wakifurahia ushiriki katika maonesho hayo Nchini Ghana.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Fedha chini ya Mhasibu Mkuu wa Serikali Bi. Miriam Mnzava alipotembelea banda la Zimbabwe wakati wa maonesho hayo. Picha zote na Scola Malinga – Wizara ya fedha, Tanzania.