Mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) manispaa ya Singida, Hassan Mazala akizungumza juzi kwenye halfa ya uzinduzi wa hotel ya ya Chemuchemu park na shina la wakereketwa wa CCM wa hoteli hiyo mpya.
Mfanyabiashara maarufu mjini Singida, Mushi Kimboka (aliyeshika kipaza sauti) akitoa taarifa yake kwa mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM (NEC) taifa Manispaa ya Singida, Hassan Mazala (aliyevaa miwani) juu ya ujenzi wake wa hotel ya Chemuchemu Park iliyoko katika Kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya Mji wa Singida.
Mkurugenzi mtendaji wa hotel ya kitalii ya Stanley Motel, Eward Malya maarufu kwa jina la Hali Ngumu akitoa nasaha zake kwenye hafla ya uzinduzi wa hotel ya Chemuchemu park iliyopo kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya mji wa Singida. Hali Ngumu amewataka wafanyabiashara kufanya biashara halali kwa bidii na kisha wabane matumizi kwa madai kuwa ‘hali ni ngumu’.
Wanachama wapya wa CCM baada ya kukabidhiwa kadi juzi na mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) taifa Hassan Mazala (hayupo kwenye picha).
Kikundi cha burudani cha Kijiji cha Manguanjuki kikitoa burudani wakati wa uzinduzi wa shina la wakereketwa wa CCM katika Hotel ya Chemuchemu Park.
Mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) taifa manispaa ya Singida,Hassan Mazala (wa tano kushoto mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa hotel ya Chemuchemu park iliypo kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya mji wa Singida. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) taifa Manispaa ya Singida, Hassan Mazala, amewahimiza wafanyabiashara wa ngazi zote kujiunga na CCM, kwa madai kuwa ni chama pekee kinachowajengea mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao kwa amani na utulivu.
Mazala ametoa wito huo muda mfupi baada ya kuzindua tawi la wakereketwa wa hotel mpya na ya kisasa ya Chemuchemu Park, iliyopo katika Kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya Mji wa Singida.
Amesema uzoefu unaonyesha wazi kwamba wafanyabiashara wamekuwa wakishirikiana na CCM kwa muda mrefu na hali hiyo inapaswa kuendelezwa kwa sababu inazinufaisha pande zote mbili.
Akifafanua zaidi amesema amani na utulivu ndio inayopelekea wafanyabiashara na Watanzania wengine wote, wafanye shughuli zao halali kwa uhuru mpana zaidi na ambao hauathiri sheria zilizowekwa.
MNEC huyo amesema CHADEMA inaonyesha ilani yake ni kupandikiza chuki, hasira, kuchonganisha watu na upotoshaji uliopitiliza, na kwa hali hiyo, CHADEMA sio mahali rafiki kwa wafanyabiashara.
Katika hatua nyingine, Mazala ametumia fursa hiyo kuwahimiza viongozi/watendaji wa CCM na wa serikali yake, kuwa karibu na wafanyabiashara ili kujua matatizo/kero wanazokabiliana nazo na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.
Kwa upande wa wafanyabiashara, amewataka wafanye kazi halali kwa bidii na kwa ubunifu mkubwa na kuhakikisha wanabana matumizi au wawe na nidhamu ya matumizi.