Kumbi za Video Zawaathiri Wanafunzi Vijijini
UTARATIBU wa baadhi ya maeneo ya nje ya miji kuonesha ‘video’ bado unachangamoto kubwa kutokana na kile kuathiri wanafunzi na watoto wengine kwa kiasi kikubwa. Uchunguzi mdogo uliofanywa na dev.kisakuzi.com umebaini maeneo mengi ambayo yanafanya biashara hizi katika Mikoa ya Morogoro na Tanga (vijijini) wateja wakubwa ni wanafunzi.
Wanafunzi hutumia muda mwingi kufuatilia picha mbalimbali zinazoeneshwa maeneo haya ikiwa ni pamoja na kutafuta fedha kwa mbinu mbalimbali ili kuhakikisha wanapata kiingilio kwenye kumbi hizo. Kwa Mkoa wa Tanga baadhi ya maeneo ya vijiji vilivyopo katika wilaya ya Korogwe shughuli hizi ni zimepamba moto kiasi cha kulalamikiwa na walimu na baadhi ya wazazi maeneo hayo. Kwa mkoani Morogoro hasa nje ya mji mchezo huu pia umeshamiri na kuteka wanafunzi.