Hafla ya Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika Nchini Ghana

Ofisa Tawala Mwandamizi wa Wizara ya Fedha Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Merkion Ndofi akimkaribisha mwananchi wa Ghana katika banda la Wizara ya Fedha.

Mkuu wa Kitengo cha Mikopo kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali Wizara ya Fedha, Bi. Christina Ngonyani akitoa ufafanuzi kwa wananchi wa Ghana juu ya umuhimu wa mikopo kwa Watumishi wa Serikalini.

Mkuu wa Kitengo cha Mikopo ya Watumishi wa Umma wa Wizara ya Fedha Bi. Christina Ngonyani akiwa na Ofisa Tawala Mwandamizi, Merkion Ndofi, wakitoa ufafanuzi kuhusu utendaji wa kazi za Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali kwa wageni waliotembelea banda la Wizara ya fedha.

Msemaji wa Wizara ya Fedha, Bi. Ingiahedi Mduma akifafanua jambo kwa, Eugene Koranteng Henaku wa Umoja wa Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Serilkali za Mitaa Nchini Ghana. Picha zote na Scola Malinga- Hazina -Tanzania

Watanzania wakipunga mikono wakati wa ufunguzi wa mikutano ya watumishi wa umma barani Afrika hapa Nchini Ghana.