OXFAM Yataja Mabalozi Kampeni ya GROW

Shamim Mwasha Fashion Blogger, ni mmoja wa mabalozi hao.


IMG_7191

Mwanasheria –Mshauri Mwelekezi katika Masuala ya Haki za Ardhi – Emmanuel Massawe akifafanua jambo kwa wageni waalikwa wakati wa hafla ya kuwatangaza rasmi mabalozi wa OXFAM katika Kampeni ya GROW nchini itakayowezesha mfumo wa chakula kuwa wa haki na salama.

Na Mo Blog Team

TAASISI isiyo ya kiserikali ya OXFAM kwa kupitia Kampeni yake ya GROW imewakutanisha pamoja masupa staa saba wa Tanzania wakiwemo Mbunge wa Kawe, Halima Mdee pamoja na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji kufanyakazi pamoja na vikundi vya wanawake wajasiriamali na wazalishaji, kwa lengo la kuhakikisha hakuna mtanzania atakayeteseka kwa njaa wakati mbinu za kilimo zinaweza kufanikiwa.

Akizungumza wakati wa kuwatambulisha rasmi mabalozi wa OXFAM kupitia kampeni hiyo, mmoja wa mabalozi hao Bi. Khadija Mwanamboka amesema kilimo sio tu ni sekta endelevu nchini Tanzania bali pia ni Nyanja inayowezesha kupatikana kwa chakula kwa familia na akiba ya chakula kwa taifa kwa kuwa asilimia 80 ya wajasiriamali nchini ni wakulima.

Nchini Tanzania takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wajasiriamali wanawake wanajihusisha na kilimo kikiwepo cha mbogamboga na matunda.

Aidha kampeni hiyo inakusudia kuendeleza na kukuza uzalishaji utakaoyafanya mazao hayo ya kilimo kuwa na bei muafaka kwa faida ya wakulima hao wa chini na wa kati.

IMG_7195

Naibu Mkurugenzi Mkazi OXFAM-Justin Morgan akziungumza na wageni waalikwa namna kampeni hiyo itakavyofanya kazi zake za uhamasishaji hapa nchini.

IMG_7224

Mabalozi wa OXFAM katika kampeni ya GROW wakati wa hafla hiyo.

IMG_7262

Khadija Mwanamboka – Mbunifu wa Mavazi akipozi na Tuzo yake mara baada ya kutangazwa rasmi.

IMG_7257

Dina Marious- Mtangazaji wa Redio.

IMG_7240

Jacob Stephen Muigizaji.

IMG_7244

Masoud Kipanya Mchora Katuni.

IMG_7280

Mabalozi wa OXFAM katika kampeni ya GROW katika picha ya pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkazi OXFAM-Justin Morgan (wa pili kushoto).

IMG_7236

Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki.