Serikali Yatangaza Kumpa Milioni 100 Atakayemtaja Aliyerusha Bomu Mkutano wa Chadema

Nembo ya Taifa

SERIKALI Imetoa kiasi cha fedha sh milioni 100 ambacho itamzawadia mtu atakaye mfichua aliyerusha bomu katika mkutano wa kampeni za udiwani za CHADEMA Mkoani Arusha. Kiasi hicho cha fedha kimetangazwa muda huu bungeni mjini Dodoma ili kuhakikisha inachochea kupatikana kwa mtu huyo.

Hata hivyo Serikali imeahidi kumsaka mtu huyo anayedaiwa kurusha bomu ambalo limesababisha kufa kwa watu wawili hadi sasa na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa. Taarifa zaidi baadae kidogo…!