Warembo Redd’s Miss Kinondoni Wafanya Usafi Hospitalini

Mratibu wa shindano la Redd’s Miss Kinondoni 2013, Ssebo akiwaongoza warembo kuchukua vifaa kwa ajili ya kuanza zoezi la kufanya usafi.


 

 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (kulia) akiwa na mratibu wa shindano la Redd’s Miss Kinondoni 2013, Ssebo wakiwaongoza warembo mara baada ya warembo hao kutembelea hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kutembelea wagonjwa na kufanya usafi.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (katikati) akiwa na mratibu wa shindano la Redd’s Miss Kinondoni 2013, Ssebo wakitoa maelekezo kwa warembo mara baada ya warembo hao kutembelea hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kutembelea wagonjwa na kufanya usafi.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (kulia) akiwagawia warembo vifaa kwa ajili ya kujikinga na vumbi mara baada ya warembo hao kutembelea hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kutembelea wagonjwa na kufanya usafi.
Warembo wajielekezana namna ya kuvaa vifaa vya kujikinga na vumbi kabla hawajaanza zoezi la kufanya usafi.
 Mratibu wa shindano la Redd’s Miss Kinondoni 2013, Ssebo akiwaongoza warembo kuchukua vifaa kwa ajili ya kuanza zoezi la kufanya usafi.
 
Warembo wa Redd’s Miss Kinondoni 2013 wakiwa katika zoezi la kufanya usafi.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (kulia) akiongea na vyombo vya habari. 
Mrembo wa Redd’s Miss Tanzania 2012/13 ambaye alitokea Redd’d Miss Kinondoni 2012 akiongea na vyombo vya habari.
  Mratibu wa shindano la Redd’s Miss Kinondoni 2013, Ssebo akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika zoezi la kufanya usafi.

Bw. Ssebo alisema kuwa mchakato wa kumtafuta Redd’s Miss Kinondoni umeanza kwa kishindo ambapo warembo hao ambao walishaanza kambi tokea mwishoni mwa wiki iliyopita jana waliweza kutembelea hospitali ya Mwananyamala  na kufanya usafi.

Warembo hao ambao wanajumuisha vitongoji vya Dar Indian Ocean, Sinza na Ubungo baada ya kufanya usafi hospitalini hapo walijionea hali mbaya iliyokuwepo pale na kuamua kufanya harambee ya kuchangisha hela kwa ajili ya kununua vitanda kwa ajili ya akina mama wanaojifungua (delivery beds).

Harambee hiyo imepangwa kufanyika siku ya alhamis tarehe 13, katika ukumbi wa Ambassador kuanzia saa moja jioni huku mgeni rasmi akiwa ni meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda.

Warembo hao leo watafanya usafi hospitali ya Sinza na kutembelea mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi.

Mashindano ya Redd’s Miss Kinondoni yanatarajiwa kufanyika June 21, huku walowa yamedhaminiwa na Redd’s Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, Mrokim Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog, DjChoka Blog na Kajunason Blog.