Twiga Stars yatua Harare kuikabili Botswana, COSAFA

Baadhi ya wachezaji wa

Harare,

Twiga Stars imewasili salama hapa Harare leo mchana kwa ajili ya michuano ya
wanawake ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA)
ambapo imefikia hoteli ya Tower Rainbow. Itacheza mechi yake ya kwanza kesho
saa 9.15 kwa saa za hapa dhidi ya Botswana.

Mchezo huo wa kundi B utafanyika kwenye Uwanja wa Gwanzura. Timu ilifanya
mazoezi leo saa 9 kujiandaa kwa ajili ya mechi hiyo.

Wachezaji ambao wanatarajia kuanza kwenye mechi ya kesho kwa mujibu wa Kocha
Charles Boniface ni; Fatuma Omari, Mwajuma Abdallah, Fulkaria Charaji, Mwanaidi
Tamba, Sophia Mwasikili (nahodha), Fatuma Bashiri, Mwanahamisi Omari, Eto
Mlenzi, Asha Rashid, Fatuma Mustafa na Fadhila Omari.

Twiga Stars itacheza mechi yake ya pili keshokutwa (Julai 3 mwaka huu) kwenye
uwanja huo huo dhidi ya Zambia kuanzia saa 6.30 mchana kwa saa za hapa. Mechi
yake ya mwisho katika hatua ya makundi itakuwa dhidi ya Afrika Kusini ‘Banyana
Banyana’ ambayo itachezwa Julai 5 mwaka huu kwenye uwanja huo huo kuanzia saa
6.30.

Regards,
Boniface Wambura
Media Officer
Tanzania Football Federation (TFF)