Zuku Pay Tv Yazindua Zuku Swahili Movies chanel


ZUKU Pay Tv imezindua Zuku Swahili Movies chaneli namba 210 ambayo ni watakua wakionesha burudani za muziki na filamu za kiswahili.

Tukio hili la kifalme lilitekwa utamaduni wa kiswahili na kuthamini historia ya filamu nchini Tanzania na kuthamini mchango wa waenzi pamoja na nyota mpya wa sekta ya filamu.
Waigizaji, wakuzaji wa filamu wa Arusha na Dar es Salaam walikaribishwa kwa kapeti nyekundu.

Akizungumza katika uzinduzi wa Zuku Kiswahili Channel, Mohammed Jenneby Mkurugenzi Mtendaji Wananchi Satellite alionyesha matumaini yake na kueleza mkakati wa biashara kwa zaidi ya wateja million mia moja katika kanda ya Afrika Mashariki. “Kiswahili ni lugha ambayo inawaunganisha wakazi wa Afrika Mashariki, Kati na Kusini. Lugha ya Kiswahili itaendeleza jukumu muhimu ya kuleta maendeleo ya kanda. Chaneli ya Zuku Swahili inasherekea maendeleo yetu na pia kukuza nje utamaduni wetu kupitia filamu duniani

Mtange wa Satelitie wa Zuku hupatikana kwa nchi 15 Afrika Mashariki na kampuni ya Wananchi inalengo la kupanua utaambazi wake kufikia nchi 40 hivi karibuni. Kampuni pia imeelezea nia yake ya kuendelea kuwekeza katika kanda ya Afrika Mashariki

Zuku Swahili Channel 210 inajivunia filamu bora, sinema na burudani ya kiswaili kutoka Tanzania na inelenga kujumuisha uzalishaji kutoka Uganda, Kenya, Rwanda na DRC katika miezi ijayo.

Zuku Kiswahili Channel 210 inaonyesha filmau, michezo ya kuigiza, majadiiano na muziki. Chaneli hii inapatikana katika vifurushi vya Zuku Poa, Zuku Classic, na Zuku Premium

Fadhili Mwasyeba, Meneja Mkuu Zuku Tanzania aliwashukuru wazalishaji na watunga filamu ambao wameshirikiana na Zuku kuzindua chaneli hii. “Kampuni inaendelea kutafuta filamu bora; nia yetu ni kununua haki za kuonyesha filamu hiii kwenye jukwaa letu la Zuku Pay TV. Tunawakaribisha watengenezaji wa filamu katika kanda ya Afrika Mashariki kutumia jukwaa letu na kufanya biashara na sisi, alisema.

“Ili kuhakikisha tunakutana na watunga filamu wote tutakuwa na msafara wa Zuku Caravan ambao utatembea kote nchini. Tunawahimiza wadau wote kukutana na kufanya biashara nasi” alisema Bw. Mwasyeba.

Ziara ya kwanza ya msafara utaanza Arusha tarehe 15 Juni Arusha na baadaye kutembelea mikoa ya Moshi, Mbeya, Iringa, Morogoro, Dodoma, Shinyanga, Bukoba na Dar es Salaam.