Wasanii Wanapoamua Kuuza Kazi Zao Wenyewe Mitaani…!
WASANII wanapoamua kuuza kazi zao wenyewe mtaani badala ya kuingia mikataba na ‘madalali’ wengine ujue kuna kitu hakija kaa sawa katika utaratibu mzima wa usimamizi wa kazi za wasanii. Wengi wanalalama kuibiwa kuanzia kwa ‘madalali’ na baadhi ya wananchi wasiokuwa waaminifu.
Juzi dev.kisakuzi.com imekutana na kundi la maigizo ya vichekesho Kashi Kashi (Maarufu kama Mizengwe) wakinadi kazi zao wenyewe maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam. Kundi hili linaundwa na wasanii kama Mkwere Original, Mzee Matata, Safina , Maringo 7 na Sumaku.