Angalia Matukio ya Shida ya Maji Kata ya Kishapu

Angalia Matukio ya Shida ya Maji Kata ya Kishapu

Na dev.kisakuzi.com, Kishapu

WANASEMA maji ni uhai, kinyume chake bila maji hakuna uhai wa mwanadamu na hata wanyama. Kimsingi kauli hii inaonesha umuhimu wa maji katika maisha ya kila siku ya binadamu na hata viumbe wengine.

Shughuli nyingi zinazofanywa na mwanadamu kila siku zinategemea uwepo wa maji. Matumizi ya maji kwa shughuli za binadamu hayaepukiki. Na hata katika mwili wa binadau ni muhimu zaidi, kama huto yaitaji maji kwa kunywa utayahitaji kwa kuoga na usafi wa shughuli nyingine.

Kwa mantiki hiyo hali yoyote ya upatikanaji ngumu ya upatikanaji wa maji unaathiri maisha ya kila siku ya mwanadamu. Shida ya huduma ya maji eneo fulani huweza kuchangia ugumu wa maisha kiasi fulani. Shida ya maji maeneo mengine huweza kupunguza shughuli za uzalishaji mali, hii ni kutokana na muda mwingi kupotezwa na jamii kwa ufuatiliaji wa maji hasa maeneo ya vijijini.

Hali kama hii ya shida ya huduma ya maji ndiyo inayowakumba wananchi wa vijiji anuai vya Kata ya Kishapu, Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga. Kata ya Kishapu ina vijiji nane yaani Mhunze, Lubaga, Isoso, Mwanuru, Migunga, Mwamagembe, Mtaga, na Kishapu yenyewe.

Japokuwa vijiji vingi vina shida kubwa ya huduma za maji, lakini hali ya ugumu wa upatikanaji huduma hizo hutofautiana kutoka kijiji kimoja hadi kingine. Kati ya vijiji vyote nane vijiji vinne ndio vyenye shida ya maji zaidi. Vijiji hivyo ni pamoja na Lubaga, Isoso, Mwanuru na Kishapu yenyewe.
Zifuatazo ni picha anuai zikionesha wananchi wanavyoangaika kutafuta huduma za maji vijiji hivyo.

Mchuuzi wa maji Kijiji cha Mhunze akichota maji kwaajili ya kuuza. Dumu moja huuza wastani wa sh 500.

Wanyama nao wanahitaji maji jioni baada ya malisho huletwa hapa.

Wanyama anuai wakinywa maji kwenye chanzo cha maji ambacho hutumiwa pia na wanakijiji.

Wakati wananchi wengine wanachota maji wengine hufua eneo hilo.

Mmoja wa wakazi wa Isoso akichota maki kwenye kisima cha muda eneo la Mto Nkonze.

Shughuli mbalimbali za usafi wa mwanadamu zikiendelea eneo la Mto Tungu.

Shida ya Maji Kata ya Kishapu haipo kwa wananchi pekee hata wanyama. Hapa nao wanapita kunywa maji baada ya malisho

Mtoto akichota maji katika kisima cha muda Mto Tungu, kijijini Mhunze.

Baadhi ya wakazi wa Kata ya Kishapu wakichota maji kwenye Mto Tungu

Utafutaji maji huitaji nyenzo za ubebaji kama toroli kutokana na umbali.

Harakati za utafutaji maji ni kila eneo Kata ya Kishapu

Wanafunzi nao baada ya shule hurudi mitaani na kusaidia familia zoezi la utafutaji maji.

Mashimo haya ni visima vya muda ambavyo kwa sasa vimekauka katika eneo la Mto Tungu.

Wanawake nyumbani ndio watafutaji zaidi wa maji, hapa mmoja wa akinadada akitoka kuchota maji kwa kutumia baiskeli.

Mwanamke akiwa kisimaji kijijini Isoso

Mmoja wa waandishi wa habari kutoka kituo cha Clouds FM, Aziz Kindamba akinywa maji kwenye kisima cha muda.

Mmoja wa waandishi wa habari kutoka dev.kisakuzi.com akinywa maji kwenye kisima cha muda.

Heka heka za utafutaji maji eneo la Mto Tungu.

Haya ni maji yaliotuwama, si salama lakini wakazi hulazimika kuyatumia kutokana na shida ya huduma hiyo.

Watoto nao husaidia familia zao kutafuta maji nyumbani kama inavyoonekana mtoto akiwa eneo la mto TUNGU

Mwanafunzi akifua eneo la chanzo cha maji Kishapu