Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa somo kwa wasichana watukutu wanaotunzwa kwenye kituo cha kurekebisha tabia zao cha Pertapis kilichoko jijini Singapore wakati alipokitembelea tarehe 6.6.2013.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa msichana anayetunzwa katika kituo cha watoto wa kike watukutu cha Pertapis kilichoko Singapore wakati alipokitembelea kituo hicho tarehe 6.6.2013. Mama Salma yupo nchini Singapore akiambatana na Rais Kikwete katika ziara ya kikazi ya siku mbili nchini humo. Kulia ni Mkuu wa kituo hicho Mama Sahnim Sokaimi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa somo kwa wasichana watukutu wanaotunzwa kwenye kituo cha kurekebisha tabia zao cha Pertapis kilichoko jijini Singapore wakati alipokitembelea tarehe 6.6.2013.
Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja kati yake na uongozi wa kituo cha kuwarekebisha tabia wanawake na wasichana cha Pertapis kilichoko huko Singapore wakati alipokitembelea tarehe 6.6.2013. Kushoto kwa Mama Salma ni Mama Badriya Kiondo, Afisa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini India. (PICHA NA JOHN LUKUWI)