Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungnao wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwasha mashine kuzindua pampu ya maji kwa wananchi wa mji wa Namanyere Wilayani Nkasi, katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani, ambapo hapa Nchini yameadhimishwa rasmi jana Mkoani Rukwa, wa pili kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk. Terezya Huvisa.
Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea mabanda ya maonesho kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani yaliyoadhimishwa jana katika Viwanja vya sabasaba kijiji Namanyere Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa.
Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia vijarida mbalimbali alipotembelea Banda la Ofisi ya Makamu wa Rais katika maonesho ya maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika jana katika viwanja vya sabasaba Namanyere Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa, kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk. Terezya Huvisa.
Kikundi cha Taarab cha TOT chini ya uongozi wa Malkia wa Mipasho Hadija Omar Kopa kikitumbuiza kwenye maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani Kitaifa yaliyoaadhimishwa jana katika viwanja vya sabasaba Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa, wa kwanza kushoto anaejirusha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk. Terezya Huvisa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia Wananchi kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani yaliyoadhimishwa Kitaifa jana katika Viwanja vya sabasaba Namanyere Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa.