Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Kimomunisti Cha Viatnam (CPV), Hoang Binh Quan, baada ya ujumbe wa CPV kuwasili asubuhi hii kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Quan na ujumbe wake wanatarajiwa kuwa na mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana baadaye leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam, Ramadhani Madabiba.
Balozi wa Vietnam Tanzania, NguyenThien akimtambulisha Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Kimomunisti Cha Viatnam (CPV), Hoang Binh Quan kwa katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Martin Shigela (kulia) baada ya kushuka katika ndege, kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Dk.Asha-Rose Migiro na mgeni wake, wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa mgeni huyo na viongozi wengine wa CCM, wakati wamapokezi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JN, Dar es Salaam.
Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza na Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Kimomunisti Cha Viatnam (CPV), Hoang Binh Quan, baada ya kumpokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere asubuhi hii. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO)