Kenya Uso kwa Uso na Cameroon Fainali za Pan African Guinness Footbal Challenge

Okraku Kofi&Isaac Aryee:- Washindi wa kwanza wa nusu fainali ya pili ya Guinness Football Challenge Emmanuel Okraku Kofi(kushoto) na Isaac Aryee(kulia) katika picha ya pamoja na waendeshaji wa kipindi hicho Larry     Asego na Mimi kalinda.
 

TIMU ya Kenya kutoka Afrika mashariki, Ephatus Nyambura na Samuel Papa walikusanya alama 14 katika mzunguko wa muundo na wakafikia hadi hatua ya penati baada ya kuishinda timu ya Cameroon.Wakiwa washindi wa pili wa mchezo bado wana nafasi ya kushinda katika fainali ya mashindano haya.Waghana Emmanuel Kofi Okarku na Isaac Aryee walifanikiwa kufikia hatua ya ukuta wa pesa wa Guinness.

Ephatus, Samuel pamoja na Emmanuel na Isaac sasa watakutana na Desmond, Jonathan, Francis Ngigi na Kepha Kimani kufanya timu nne katika fainali ya Pan-African. Hawa wote wana nafasi ya kupeperusha bendera ya nchi zao, lakini watahitaji kujiandaa vizuri na kuwa makini ili waweze kushinda taji la Pan-African Guinness Football Challenge.

Watakaokutana katika fainali ya mashindano ya Pan-African GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE watakuwa ni timu mbili kutoka Afrika mashariki na mbili kutoka Afrika magharibi. Kutoka Afrika mashariki ni Ephatus Nyambura, Samuel Papa, Francis Ngigi na Kepha Kimani.
Ushindani kati ya Afrika Mashariki na Afrika Magharibi utakuwa mkali,ni upande upi wa bara utakaoshinda taji hili?

Fainali ya mashindano ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, yanayoandaliwa na Endemol , itarushwa na televisheni za ITV na Clouds TV siku ya Jumatano saa 3:15 usiku ITV na saa 2:15 usiku Clouds TV kwa hiyo hakikisha unaangalia mchezo huu huku ukiburudika na kinywaji cha GUINNESS.

Usikose kufuatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.