Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa

Bendera ya Tanzania ikipandishwa pamoja na ile ya umoja wa mataifa (UN)

 

IMG_0231

 Mgeni rasmi Waziri Mambo ya Ndani nchini Dk. Emmanuel Nchimbi, Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan na Kanali Dominic Mrope wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakitoa heshima kwa wimbo wa mataifa kwenye maadhimisho hayo.

IMG_0259

Mgeni rasmi Waziri Mambo ya Ndani nchini Dk. Emmanuel Nchimbi akielekea kuweka shada la maua kwenye Mnara wa Mashujaa ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka askari wa kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa walipoteza maisha wakiwa kazini.

 

 

IMG_0271

Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akielekea kuweka shada la maua kwenye maadhimisho ya kuwakumbuka Askari wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika leo kwenye mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa uliopo viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar.

IMG_0281

Kanali Dominic Mrope wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akiweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa kwa niaba ya Meja Jenerali Salum Mustafa Kijuu wakati wa maadhimisho ya siku ya kuwakumbuka Askari wa kulinda Amani wa Umoja wa mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja leo.

IMG_0284

Kanali Dominic Mrope wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akitoa heshima zake mara baada ya kuweka shada la maua.

IMG_1145

Mmoja wa askari wa JWTZ akipendisha bendera ya Umoja wa Mataifa kama ishara ya kumbukumbu ya Askari wa Umoja huo wanaolinda Amani katika nchi mbalimbali za Afrika.IMG_0433

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wageni waalikwa wakati wa maadhimisho ya kuwakumba Askari wa Umoja wa mataifa wa Kulinda Amani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

IMG_0374

Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akizungumza kwa niaba ya Mratibu Kazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini Dk. Alberic Kacou kwenye maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda Amani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

IMG_0389

Zainab Abdallah moja ya Vilabu vya Umoja wa Mataifa akighani shairi wakati wa maadhimisho hayo.

IMG_0406

Baadhi ya Askari wa Umoja wa mataifa wa Kulinda Amani wakati wa maadhimisho hayo.

IMG_0407

IMG_0192

 

Mkuu wa uendeshaji na ushauri wa Ofisi za Umoja wa Mataifa Tanazania Bw.George Otoo (wa pili kulia) na   Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu (kulia) wakiwa na baadhi ya maafisa mbalimbali wa jeshi la Tanzania wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye maadhimisho hayo.

IMG_0394

Kushoto ni Usia Nkhoma Ledama wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na baadhi ya mabalozi na maafisa mbalimbali wa jeshi nchini.

 

 

IMG_0464

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani  ya nchi Dk. Emmanuel Nchimbi akipeana mikono na Askari Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani kutoka Tanzania kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

IMG_0487

Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akisalimiana na Askari wa Kulinda wa Umoja wa Mataifa waliohudhuria maadhisho hayo leo jijini Dar es Salaam.

IMG_0542

Askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda Amani kutoka Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja.

IMG_0554

Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akibadilishana mawazo na mmoja wa askari wa Vikosi vya  Umoja wa Mataifa vya kulinda Amani wakati wa maadhimisho hayo.

Na Mwandishi wetu.