Tanzania Yavuna Dola 5,500 Guinness Footbal Challenge

Tanzania Yavuna Dola 5,500 Guinness Footbal Challenge

TUMEONA nusu fainali ya kwanza ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLEGE™ ambapo timu ya Ghana walionesha kuwa wao ni timu bora baada ya kushinda na kuwa timu iliyoshinda kiasi kikubwa zaidi cha pesa.

Jonathan Nabb na Desmond Odaano walionesha kuwa wana uwezo na ni majasiri walipowashinda adui zao na mwisho kushinda hadi $12,000 USD baada ya kulenga lengo namba nne katika hatua ya pesa ukutani.

Watakaorudi nyumbani ni Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad kutoka Dar-es-Salaam wakiwa na $5,500 USD walizojipatia katika hatua za kitaifa.Sasa kazi itakuwa kwa timu mbili za Kenya katika nusu fainalli ijayo watakapokuwa wakiiwakilisha Afrika mashariki.

Washindi,Jonathan na Desmond,walizawadiwa pia $4,000 USD baada ya kuonesha mchezo mzuri sana katika mizunguko miwili ya mwanzo ya mchezo ambapo hawakukosa hata swali moja.Sasa wamefanikiwa kujihakikishia nafasi katika fainali ya Pan-african na hata kuwa washindi wa mashindano hayo.

Watakaowaunga washindi ni Francis Ngigi na Kepha Kimani kutoka Nairobi waliokuwa washindi wa pili.Japokuwa hawakufanikiwa kufikia hatua ya pesa ukutani lakini wamefuzu fainali.Wenzao kutika Kenya Kenneth Kumau na Wills Ogutu hawakufanikiwa kufuzu hivyo Francis na Kepha ndio watakaowakilisha Afrika mashariki.

Mkurugenzi wa GUINNESS alisema,”Sote Tanzania tunawapongeza Daniel na Mwalimu-japokuwa hawakufanikiwa kufuzu fainali lakini wamejishindia kiasi kikubwa cha pesa.Kila timu ilijitahidi kufikia nusu fainali na hongera kwa Desmond na Jonathan kutoka Ghana kwa ushindi wao.Sasa tunasubiri nusu fainali ijayo kila la heri kwa wote pamoja na timu za Kenya zitakazowakilisha Afrika mashariki.

Vying for their chance in the Finals in the second Semi-Final are the following football fanatics:

AFRICA MASHARIKI

• JEZI NYEUSI – Ephatus Nyambura,24 na Samuel Papa,23 kutoka Nairobi watatarajia kushinda zaidi ya $3,000 USD walizopata katika hatua za kitaifa na robo fainali.Ephatus atajibu maswali wakati Samuel anayechezea Nakuru Allstars atakuwa mchezaji.

• JEZI NYEKUNDU – Kenneth Mukuri,26 na Chris Mwamgi,19 kutoka Nairobi watakuwa wakitarajia kushinda zaidi ya $1,500 USD walizopata katika hatua za kitaifa.Kenneth atakuwa kichwa cha timu wakati Chris atakuwa mchezaji.

CAMEROUN:

• JEZI ZA KIJANI – Emerald Tchouta,24 na Abdul Sam,25 ambao wana jumla ya $6,500 baada ya kulenga lengo namba nne katika robbo fainali.Sasa Emerald na Abdul watacheza kuwania nafasi ya kufuzu fainali.

GHANA:

• JEZI ZA BLUU – Emanuel Kofi Okarku,27 na Isaac Aryee,25 kutoka Accra Ghana wataichezea nchi yao kutoka Afrika magharibi ili kufuzu fainali.Tayari wana $3,000 USD hivyo Isaac atahitajika kuonesha kipaji chake cha kucheza wakati Emanuel atajibu maswali.

Mashabiki wa mashindano haya wanaweza kupima maarifa yao kupitia mchezo wa simu za mkononi wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE unaopatikana katika simu za kijamii za GUINNESS kwa ajili ya wapenzi wa mpira wa miguu, GUINNESS® VIP™. Jiunge bure sasa upime maarifa yako katika michezo,tembelea m.guinnessvip.com sasa.

Make sure to like to GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE Facebook page for all the latest details – www.facebook.com/[insert]

Nusu fainali ya pili ya mashindano haya itaoneshwa ITV jumatano saa 3:15 usiku, usiikose huku ukiburudika na Guinness.

Tafadhali kunywa kistaarabu-kwa wenye miaka 18 na kuendelea tu.