Mataifa ya Afrika yanasherehekea miaka 50 tangu kuundwa kwa umoja wa nchi huru za Afrika , OAU, 25.05.2013 jumuiya iliyokusudiwa kuleta umoja wa bara hilo.
Mfalme Haille selassie wa Ethiopia na wakuu wa nchi na serikali 31 walikutana mjini Addis Ababa tarehe 25, mwezi wa Mei kuizindua jumuiya hiyo mwaka 1963. Uzinduzi wa OAU , Umoja wa nchi huru za Afrika miaka 50 iliyopita unaadhimisha hatua muhimu ya kihistoria kwa bara zima, ambalo lilikuwa wakati huo likipitia kwa haraka katika kipindi cha kutoka katika ukoloni.
Wengi wa viongozi ambao walikuwapo wakati huo wameweza hivi karibuni tu kujitenga na hisia za kikoloni na wanatafuta njia kwa nchi zao kujenga upya mifumo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi iliyoporomoka kwa kutaka kushirikiana zaidi na majirani zao.
Upande wa kusini , makoloni ya Ureno ya Angola na Msumbuji bado yanakabiliwa na hali ya kujitoa kutoka katika zaidi ya muongo mmoja wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Hatua hiyo ni ndefu zaidi kwa hali ya baadaye ya Zimbabwe na Namibia, ambapo nchi hiyo ilikuwa inadhibitiwa na Afrika kusini ya kibaguzi wakati huo, na ilichukua zaidi ya miaka 30 kabla ya Afrika kusini binafsi kufikia serikali ya kidemokrasia.
Mkusanyiko huu wa kihistoria 25.05.2013 ni ishara ya ndoto za bara ambalo limenyonywa vya kutosha.
Kwa Waafrika wengi ndoto hizo bado hazijatimia licha ya matumaini ya muda huo na juhudi kubwa tangu wakati huo.
Katika hotuba yake kwa viongozi waasisi wa OAU, Haille Selassie alikumbusha udhalilishaji uliofanyika hapo kabla.
“Kipindi cha ukoloni ambacho tulitumbukizwa , kilitufikisha mahali bara hili kudhibitiwa na wakoloni , na watu wetu ambao walikuwa huru na wenye kujisikia fahari kudhalilishwa na kuwa watumwa.” amesema.
“Leo Afrika imejitokeza kutoka katika njia hii ya giza. Mapambano yetu dhidi ya uovu yamekwisha.
Hali hii ilikuwapo katika baadhi ya sehemu za Afrika, ikiwa ni pamoja na Ethiopia yenyewe.Mfalme alitangaza kuwa bara hilo liko njiani kati ya Afrika ya kale na Afrika ya hapo baadaye. Wengi wangesema kuwa hali hiyo bado imeendelea hata baada ya miaka 50.
Waafrika wengi bado wana uhaba wa chakula na wanaishi katika umasikini uliokithiri. Mabadiliko ya hali ya hewa yameleta ukame na mafuriko. Ukosefu wa ajira ni mkubwa, huku kukiwa na matumaini machache kwa vijana katika maeneo mengi ya bara hilo.
Vita na mizozo
Mapigano yanaendelea nchini Mali, jamhuri ya kidemokrasi ya Congo na Sudan.
Wanadiplomasia wa Afrika wanasema mradi wa kuiunganisha Afrika kuwa bara lenye amani si jambo lililoshindwa lakini ni hatua inayoendelea.