Msigwa Afikishwa Mahakamani Iringa kwa Uchozizi, Aachiwa kwa Dhamana…!

Wafuasi wa Chadema wakiwa wamembeba Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa baada ya kuachiwa kwa dhamana jana.

Watuhumiwa wa vurugu za Iringa wakishuka kwenye gari walipofikishwa katika mahakama ya Iringa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.

Mchungaji Peter Msigwa na mbunge wa Iringa Mjini Chadema akishuka kwenye gari la Polisi baada ya kufikishwa mahakamani jana.

SAKATA la vurugu za machinga na Polisi mjini Iringa limechukua sura mpya baada ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kumfikisha mahakamani mbunge wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji, Peter Msigwa pamoja na watuhumiwa wengine zaidi ya 70. Huku mahakama hiyo ikitoa masharti nafuu ya dhamana kwa watuhumiwa hao na kuwaonya kutofanya kosa kwa kipindi chote cha kesi hiyo inapoendelea kusikilizwa.

Watuhumiwa hao  walifikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa Mheshimiwa Godfrey Isaya  leo  majira ya saa 8 mchana  huku wakiwa  chini ya ulinzi mkali  wa askari  wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) waliokuwa na msafara  wa magari zaidi ya matatu  likiwemo  gari ya maji ya  kuwasha .

Mbali ya mbunge Msigwa  kupanda gari ndogo  ya  wazi ya  polisi pamoja na  watuhumiwa  wawili wanawake  waliokamatwa katika  vurugu  hizo bado  watuhumiwa  wengine 74  walitumia usafiri wa karandinga la polisi .

 Mbele  ya mahakama  hiyo  wakili  wa serikali  Adolph Maganda alisema  kuwa  watuhumiwa hao kwa pamoja  wanatuhumiwa  kwa kosa kwa makosa matatu  likiwemo la kufanya kushiriki  mkutano na kufanya   vurugu ,uchechezi na kuharibu mali kinyume na sheria 

Huku mbunge  akisomewa mashitaka mawili likiwemo  kushawishi   na kufanya mkutano bila  kibali  .

Watuhumiwa  wote  wamekana  mashitaka  dhidi yao  huku  wakili  wa  serikali akidai  kuwa hana pingamizi na dhamana kwa  watuhumiwa hao wote  hata  hivyo wote   wamekana  mashitaka  yote yaliyotolewa  dhidi  yao .

Hata  hivyo makimu anayesikiliza kesi  hiyo alisema kuwa dhamana kwa  washitakiwa  wote  ipo  wazi  kwa kila mmoja kuwa mdhamini mmoja anayeaminika pamoja na kusaini hati ya dhamana  ya Tsh milioni moja .

 Hadi majira ya  saa 10 jioni mahakama  hiyo  ilikuwa ikiendelea na mchakato  wa  kupitia barua  za dhamana kwa  wadhamini  huku  mbunge akiwa  wa kwanza kudhaminiwa ,mbali ya  mbunge  watuhumiwa kati ya 74  waliokuwa  bado kupata  wadhamnini  ni  watuhumiwa  sita pekee.

 Katibu  wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) wilaya ya Iringa mjini Suzana Mgonakulima alisema  kuwa  mchakato  wa  kuwadhamini  watuhumiwa  wote  waliosalia unaendelea kufanyika na kuwa wana uhakika wa  watuhumiwa  wote kudhaminiwa .

Hadi majira haya ya saa 10:40 mbunge msigwa na wengine  wameachiwa  huku  watuhumiwa 26 kati ya 74 wamekosa dhamana hadi kesi hiyo itakapotajwa  tena tarehe 3 /6/2012
Wakati huo huo wananachi  waliofika mahakamani hapo  kushuhudia mbunge  wao akifikishwa mahakamani wamempongeza mkuu  wa  kikosi cha kutuliza ghasia mkoa  wa Iringa (FFU) Said Abdulah Mnunka  kwa kusimamia amani na utulivu katika  eneo hilo la mahakama na jinsi ambavyo alivyoweza  kupambana na machinga  pasipo kumwaga damu kwa  siku ya  jana wakati  wa vurugu  hizo.
CHANZO: Picha na Habari kwa Hisani ya Francis Godwin