Rumadha: Kutoka Uswahilini Hadi Ughaibuni

Sensei Rumadha na mkewe Anita pamoja na mdogo wake Rumadha, Kibwana Fundi katika shangwe

Sensei Rumadha Fundi (mstari wa nyuma) akiwa na wataalamu wenzie wa mapafu

SENSEI Rumadha Fundi amefanikiwa kujiongezea taaluma kutoka Usensei wa Karate na Mwalimu wa Yoda na sasa kufikia kuwa mtaalamu wa tiba za binadamu upande wa mapafu! Huyu si mwingine bali ni Mtanzania mtaalamu wa michezo ya Karate na Yoga Sensei Rumadha Fundi (3rd Dan, Black Belt) mwenye maskani yake kule nchini 
Marekani. 

Mai 17, 2013 Sensei Rumadha Fundi akishangiliwa na kupongezwa na ndugu na marafiki waliomshuhudia akipokea shahada ya ‘Associate in Applied Science Cardiopulmonary Respiratory Care’ kutoka Collin College, McKinney, Texas, nchini USA.

Sensei Rumadha anafanikiwa kuongezea CV yake kwa kula nondo ya utaalamu wa tiba za mapafu na moyo. Sensei Rumadha sasa amekuwa mtaalam Respiratory Therapist: Mtaalam wa hewa na gasi ya kupumua, anayetibu mapafu na moyo chini ya maelekezo ya mganga wa mapafu ‘pulmonalogist’. Pia, Respiratory therapist anamajukumu mengi kama kuwatibu wagonjwa wa pumu, COPD, Ephysema, Asthma, TB na majonjwa yote yanayohusu mapafu na moyo.
 
Pia, anauwezo wa kutafsiri damu baada ya kupima hali yamgonjwa kama ana oxygen ya gas inahitaji tiba yeyote. Kwa mengi zaidi  kuhusiana na utaalam wa Respiratory Therapist fuata Link ile ipo mwisho wa “Who is Respiratory Therapist? http://en.wikipedia.org/wiki/Respiratory_therapy

Kumjua zaidi Sensei Rumadha Fundi bofya http://dartalk.com/2013/04/22/sensei-rumadha-fundi-romi-mtaalam-wa-ngazi-za-juu-wa-karate-na-yoga%E2%80%A6/