Tigo yajizatiti na mawasiliano ya intaneti Sabasaba

Jackson Mmbando na Boaz msimamizi huduma kwa wateja.

Katika jitihada zake za kuhakikisha kuwa wateja wake wanapata huduma bora za mawasiliano wakati wa maonyesho ya 35 ya biasahara ya kimataifa ya saba saba, kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imeweka mtambo wa kisasa wa intaneti aina ya 3.5G utakaotumika wakati wote wa maonyesho hayo,

Afisa uhusiano wa Tigo Jackson mmbando alisema jana kuwa mtambo huo wa kisasa ambao una spidi ya kasi katika mawasiliano ya intaneti unatoa fursa kwa watumiaji wa huduma ya intaneti katika banda lat Tigo wakati wa maonyesho hayo ya biashara yanayoendelea kwa sasa jijini Dar salaam katika viwanja vya mwalimu Julius Nyerere.

Tumeamua kufanya hivi kwasababu wakati wa maonyesho haya ya biashara kunakuwa na msongamano wa watu wengi, tuna imani kuwa mtambo huu utasaidia kurahisisha mawasiliano wakati wa maonyesho ya biashara ya mwaka huu,” alisema

Alisema kuwa watu wakataotembelea banda la Tigo wataweza pia kupata huduma ya intaneti bure bila malipo yoyote na kuongezea kuwa msimu huu kuna chumba maalum kwa ajili ya huduma ya bure ya intaneti.

Mbali na huduma ya inateneti, Mmbando alisema kuwa bidhaa zoteza Tigo zitauzwakatika bei ya chini ili kutoa nafasi kwa watanzania wengi kujiunga na mtandao huo ambao alisema kuwa kwa sasa unatoa huduma kwa bei rahisi.

Alizitaja bidhaa za Tigo ambazo zitapatikana kwa bei ya chini kuwa ni pamoja na modem za intaneti, simu za mkononi. Halikadhalika mteja atakaponunua kitu kutoka biudhaa yoyote kutoka Tigo atapata nafasi ya kushiriki katika bahati nasibu ambapo atajishindia zawadi mbalimbali.