Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba Maendeleo na Makazi, Goodluck Ole Medeye ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi akiweka jiwe la msingi katika darasa lililojengwa kwa msaada wa wafadhili toka Marekani kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya Maingi ya Oldonyowas iliyopo kata ya Oldonyosambu, wilayani Arumeru, Arusha juzi.
Madarasa ambayo yamejengwa kwa msaada na wafadhili kutoka Marekani.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba Maendeleo na Makazi, Goodluck Ole Medeye akiwapa zawadi ya kimila wafadhili waliojenga darasa katika shule hiyo inayokabiliwa na tatizo la upungufu wa madarasa kutokana na wingi wa wanafunzi ambapo kuna madarasa 7 wakati mahitaji yakiwa ni madarasa 12.
Naibu Waziri akipewa zawadi na mzee wa kimila “laigwanan” wa kijiji cha Oldonyowas kama shukrani wka kutambua mchango wake katika kusaidia sekta ya elimu kijijini hapo, kushoto ni Diwani wa kata hiyo Ealisante Nassari (Chadema)
Wafadhili wakifurahia mara baada ya kupewa zawadi na uongozi wa shule hiyo
Wanafuzni wakishuhudia hafla ya uwekwaji wa jiwe la msingi