Twiga Stars kuangwa leo TFF

) saa 7 mchana kwenye ofisi za TFF
kabla ya safari yake ya Julai Mosi kwenda Harare kushiriki michuano ya COSAFA.

Twiga Stars inayofundishwa na Kocha Charles Boniface akisaidiwa na Nasra Mohamed itaondoka saa 11 alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi ikiwa na msafara wa watu 26.

Katika msafara huo wachezaji ni 19 huku benchi la ufundi likiwa watu wanne.
Kiongozi wa msafara ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake
Tanzania (TWFA) Lina Mhando ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Twiga Stars inashiriki michuano hiyo ya Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu
Kusini mwa Afrika (COSAFA) ikiwa timu mwalikwa. Jumla ya timu nane zinashiriki
wakiwemo wenyeji Zimbabwe.

Nyingine ni Lesotho, Botswana, Afrika Kusini, Zambia, Msumbiji na Malawi. Twiga
ambayo iko kundi A pamoja na Zimbabwe, Lesotho na Botswana itacheza mechi yake
ya kwanza Julai 2 mwaka huu dhidi ya Botswana kwenye Uwanja wa Gwanzura.

Siku inayofuata itacheza na Lesotho kwenye Uwanja wa Rufaro kabla ya kumaliza
mechi za makundi Julai 5 mwaka huu kwa mechi dhidi ya wenyeji kwenye Uwanja wa
Gwanzura.

Hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo itafanyika Julai 7 mwaka huu. Kila kundi
linatoa timu mbili kuingia katika hatua hiyo na nusu fainali zote pamoja na
fainali zitachezwa Uwanja wa Rufaro.