NA MAGRETH KINABO- MAELEZO, DODOMA
8/5/2013
WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa utafiti wa chanjo ya ugonjwa wa Ukimwi ijulikananayo kwa jina la TAMOVAC -01 katika mkoa wa Mbeya unaoendelea na imeonesha kwamba ni salama na ina uwezo wa kusisimua mwili na kuzalisha viini kinga katika dozi ndogo.
Alisema utafiti huo unaofanywa na Taasisi ya Magonjwa ya Binadamu umewashirikisha watu 60.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma wakati Waziri huyo akiwasilisha hotuba yake kuhusu Makadrio ya Mapato na Matumizi ya fedha kwa mwaka 2013/2014 ya sh. 753,856,475,000 ambapo aliomba Bunge lijadili kuidhinisha.
Aliongeza kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2012/2013 wizara yake ilipanua huduma za kinga, matunzo na tiba kwa ajili ya huduma za VVU/Ukimwi.
Vituo vya kutolea huduma ya mantunzo na tiba vimeongezeka kutoka vituo 956 mwaka 2011 hadi kufikia 1,176. Jumla watu 1,135,348, wanaoishi na VVU wameandikishwa kupata huduma za matunzo,kinga na tiba.
Hivyo kati ya idadi hiyo wanaopata dawa za kupunguza makali ya VVU ni 663,884 na imeweza kutuoa huduma za wagonjwa wa majumbani kwa wanaoishi na VVU 239,298.