Ziara ya Mama Salma Kuwait

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifurahia kazi za mikono zinazofanywa na watoto wenye ugonjwa wa akili (autism) wakati alipotembelea Kuwait Autism Center huko nchini Kuwait tarehe 6.5.2013. Mama Salma amefuatana na Rais Kikwete katika ziara ya siku tatu ya kiserikali nchini humo

Baadhi ya watoto wenye ulemavu wa akili wanaolelewa katika kituo cha Kharafi Kids Activity Center kilichoko huko Kuwait wakishiriki katika ufumaji wa nguo na vitambaa mbalimbali kama anavyoshuhudia Mama Salma Kikwete alipotembela kituoni tarehe 6.5.2013

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana rasmi na Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Kharafi Kids Activity Center Bibi Sabeeka Al Jaser mara baada ya kutembelea kituo hicho kilichoko Kuwait City