Na Immaculate Makilika- Maelezo
Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano umeanza kutumika tangu mwezi July,2010, ambapo hadi kufikia Machi Mwaka huu makampuni 7 ya Mawasiliano (Telecom Operators) ya hapa nchini yameunganishwa kwenye Mkongo huo.
Hayo yamesemwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Charles Muhangwa , alipokuwa akijibu swali la Margareth Agnes Mkanga (Viti Maalum-CCM),lililouliza Je,ni lini Mkongo huo utaanza kutumika?
Muhangwa alisema kwamba kutumika kwa Mkongo huo, kumesaidia katika kushusha gharama za mawasiliano kwa mfano gharama za kusafirisha masafa(transport charges) zimeshuka kwa silimia 99 kutoka Dola za Kimarekani 20,000.00 kwa mwezi kwa umbali wa kilomita 1,000.00 kwa mwendo kasi ya 2 Megabites mwaka 2009 hadi kufikia Dola za Kimarekani 160.00 kwa mwezi kuanzia mwaka 2011 na huduma za Internet zimeshuka kutoka sh 36,000/= kwa Gigabyte(GB) moja (2009) hadi sh 9,000/= kwa GB moja(2013),sawa na kushuka kwa asilimia 75.
Aliendelea kujibu swali la tatu la Mkanga alilouliza je, ni jinsi gani Serikali imejiandaa katika kuwawezesha wananchi jinsi ya kunufaika na matumizi ya Mkongo huo,Naibu Waziri huyo ,alisema Serikali inaendelea na jitihada za kizihamasiha taasisi ambazo bado hazijajiunganisha katika Mkongo ili ziweze kunufaika na faida zilizopo.
Aidha alizitaja changamoto kubwa iliyopo hivi sasa ni uwezo mdogo wa kifedha uliopo katika wizara,Idara,Vyuo,Mashule,Hospitali na Taasisi nyingi nchini hususan za umma zikiwemo Halmashauri za miji na wilaya .
Hata hivyo Muhangwa alisema awamu ya tano ya Mradi inalenga kusaidia kutatua tatizo hili kwa kuziunganisha Wizara,Idara,Vyuo,Mashule,Hospitali na Taasisi nyingi nchini hususan za umma.
Pia alihimiza watoa huduma za mawasiliano nchini kutumia fursa hii ya uwepo wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili wajiunganishe na watumie kikamilifu (fully utilize) katika kutimiza lengo la Serikali la kuwapatia wananchi huduma bora za uhakika na kwa gharama nafuu kwa maendeleo ya Taifa letu.
Aidha makampuni ya simu ya MTL ya Malawi,UCOM ya Burundi,MTN ya Rwanda na kampuni ya simu ya MTN na Airtel za Zambia zinat