Na Immaculate Makilika- Maelezo
SERIKALI imesema inatekeleza miradi ya kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam yenye thamani ya sh. bilioni 876.336 katika barabara ya Al Hassan Mwinyi ambapo watumiaji wa barabara hiyo hutumia takribani saa moja na nusu kufika Osterbay polisi hadi daraja la Salender hususani mida ya asubuhi saa moja hadi saa tatu.
Hayo yalisemwa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge Naibu wakati akijibu swali Mbunge wa Jimbo la Temeke Abasi Zuberi Mtemvu lililouliza kuwa Je,Serikali inaweza kutoa ufafanuzi juu ya ufumbuzi wa tatizo la msongamano huo?
Alisema kuwa inayolenga kutatua tatizo hilo ,ikiwemo miradi ya kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo ambayo ni kama ifuatavyo;.Barabara ya Kimara –Kivukoni (fire),Fire-Kariakoo na Magomeni –Morocco (Sh. bilioni 240),Karakana na vituo vya mabasi yaendayo kwa haraka (BRT) pamoja na kuhamisha nguzo za umeme(sh. bilioni 47.90).
Nyingine ni Barabara ya Mwenge – Tegeta(sh. bilioni 88.00),Barabara ya Kilwa (Kilwa Road) Bendera Tatu-Mbagala Rangi Tatu ,(sh. bilioni 35.16),Daraja la Kigamboni (sh. 214.64).Flyover ya TAZARA,Serikali ya Japani imetoa msaada wa fedha kwa ajili ya usanifu,.Barabara ya Gerezani (Bendera –Tatu-KAMATA),Serikali ya Japani imetoa msaada wa fedha kwa ajili ya ujenzi.
Barabara ya Mandela (sh. bilioni 61.25) na.Barabara ya Wazo Hill –Bagamoyo-Msata (sh. bilioni 89.61).
Waziri huyo alisema ujenzi wa mabasi yaendayo haraka(BRT) kutoka Morocco kwenda Magomeni hadi Kivukoni na Kimara yatapunguza msongamano wa magari kati ya Osterbay Polisi na Daraja la Salender.
Aliongeza kuwa katika mipango ya baadae ,Serikali itaangalia uwezekano na kujenga barabara ya juu (viaduct) pande zote za daraja ,kujenga daraja lingine pembeni mwa daraja la Salender au kujenga njia mbadala (salender bridge Bypass) kutokea Kenyata Drive kuunganisha na Ocean Road..