Dk. Bilal Atoa Mkono wa Pole kwa Familia ya Balozi Habib Suleiman

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mjane wa Balozi Habib Suleiman Bibi Moza Habib, wakati alipokwenda nyumbani kwa Marehemu Kilimani mjini Zanzibar kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa wafiwa Mei 04- 2013. Kushoto ni Mama Zakia Bilal na kulia Mama Asha Bilal.