JK Atembelea Familia ya Alfred Tandau

Rais-Dkt-Jakaya-Mrisho-Kikwete-akiweka-saini-kitabu-cha-maombolezo- nyumbani-kwa-Waziri-wa-zamani-Mjumbe-wa-halmashauri-Kuu-ya-Taifa-Nec

 

 

Taifa (Nec) na Mweka Hazina wa Taifa wa CCM wa zamani, Marehemu Alfred Tandau,” width=”640″ height=”450″ class=”size-full wp-image-32208″ />Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma KLikwete wakiwafariji wafiwa nyumbani kwa Waziri wa zamani, Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na Mweka Hazina wa Taifa wa CCM wa zamani, Marehemu Alfred Tandau, aliyefariki dunia juzi jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa  amelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya tumbo[/caption]

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete Alhamisi, Mei 2, 2013, amekwenda nyumbani kwa Marehemu Alfred Tandau kuwajulia hali na kuwapa pole wafiwa kutokana na kifo cha kiongozi huyo wa zamani wa Wafanyakazi, Waziri wa Serikali na Mweka Hazina wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo  nyumbani kwa Waziri wa zamani, Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na Mweka Hazina wa Taifa wa CCM wa zamani, Marehemu Alfred Tandau, aliyefariki dunia juzi jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa  amelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya tumbo.

Rais Kikwete akiwa ameandamana na Mama Salma Kikwete amewasili nyumbani kwa marehemu Magomeni, Dar Es Salaam saa 12:45 jioni akatia saini Kitabu cha Rambirambi na kuwapa pole wafiwa akiwamo mjane wa Marehemu, Mama Margaret Tandau.

Rais ambaye mara tu baada ya kutokea kwa msiba huo aliitumia Salamu za Rambirambi familia ya Marehemu Tandau kupitia kwa Katibu Mkuu wa CCM, Mheshimiwa Abdulrahaman Kinana, alitumia kiasi cha dakika 35 kuzungumza na wafiwa.

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, na Mama Salma Kikwete, wakitambulishwa kwa watoto wa Waziri wa zamani, Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na Mweka Hazina wa Taifa wa CCM wa zamani, Marehemu Alfred Tandau nyumbani kwa marehemu Magomeni jijini Dar es salaam walipofika kufariji wafiwa

Rais Kikwete amejulishwa kuwa Marehemu Tandau ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi cha NUTA na baadaye JUWATA, Waziri wa miaka mingi katika Serikali na Mweka Hazina wa Taifa wa CCM atazikwa keshokutwa, Jumamosi, kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar Es Salaam.