Zaidi ya Milioni 700 Kushindaniwa kutoka Serengeti Premium Lager
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti katika juhudi zake za kutambua na kuthamini wateja wake, leo imezindua promosheni ambayo inaendana na kampeni yake kuu inayoendelea ya TUPO PAMOJA. Tupo Pamoja ni kampeni inayotambua wateja na kusherehekea nao pamoja. Mteja anaweza kujishindia kuanzia shilingi elfu kumi hadi million moja na pia anaweza kujipatia bia ya bure papo hapo. Kampeni hii inatarajiwa kuendeshwa kwa miezi mitatu ijayo.
Katika promosheni hii ya winda na ushinde, mteja atakapo nunua bia ya Serengeti ataweza kupata maelezo chini ya kizibo kama ilivyo kuwa katika kampeni iliyopita ya vumbua hazina chini ya kizibo.
Atapata namba maalum ambayo atatuma kwa njia ya sms kwa namba maalum na papo hapo atapata ujumbe utakao mjulisha ameshinda kiasi gani au kama amejipatia bia ya bure. Kama kawaida ili kuhakikisha ushindi huu ni wa ukweli na uhakika, promosheni hii itasimamiwa na Bodi ya Bahati Nasibu ya Taifa, kampuni mahiri ya PWC na kuendeshwa na Push Mobile.
Akizungumza alipokuwa akiwakaribisha wageni na waandishi wa habari katika hafla fupi ya kuzindua promosheni hii ya Winda na Ushinde iliyofanyika katika kiwanda cha kampuni hiyo kilichopo Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Ephraim Mafuru alisema kwamba bia ya Serengeti lager ni bia inayo jail na kuwatambua wateja wake kwa kiasi kikubwa.
“Kampeni na promosheni zetu zinalenga haswa kuwashukuru na kuwanufaisha wateja wetu, Winda na Ushinde itabadilisha maisha ya watu wengi. Bia hii inatambua umoja na ushirikiano uliopo baina yetu na hivyo basi, tunazindua promosheni ambazo zawadi zake ni utoaji wa kweli na kuwafanya wateja wetu kujisikia kwamba wanathaminiwa kwa njia moja au nyingine,” alisema Bw. Mafuru.
“Wateja wetu ndio wametuwezesha kufika tulipo. Bia hii ya Serengeti imeweza kujinyakulia tuzo za kimataifa za DLG na hapa nchini imeweza kuwa ndio bia pekee inayotengenezwa kwa kimea halisi na hivyo kupendwa na wengi. Kwa kuzingatia kanuni za kampuni yetu ambazo zinalenga kuinua maisha ya wananchi wetu, na kwa kampeni hii pia tumezingatia hilo. Zawadi zitakuwa kwa pesa taslimu ili kuwawezesha wateja wetu kujiinua kimaisha.
“Katika utendaji kazi wetu, kampuni ya bia ya Serengeti ipo karibu sana na wateja wake. Tunajenga uhusiano mzuri na kuweza kutambua mahitaji yao. Tunaelewa kwamba sio rahisi kuwafikia na kuwahudumia wateja wetu wote kwenye mahitaji yao ila tunajaribu kila tuwezalo kuchangia katika kubadilisha maisha ya jamii inayotuzunguka.
Tuna miradi mbalimbali ya kijamii kama vile maji katika mikoa mbalimbali hapa nchini. Tuna mradi mkubwa wa macho Hospitali ya KCMC Moshi na pia tunafadhili wanafunzi katika vyuo vikuu hapa Tanzania,” alieleza Bw. Steve Gannon, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bia ya Serengeti.
“Hapa katika kampuni ya bia ya Serengeti tuna angalia sana zawadi tunazotoa. Je zinasaidia wananchi katika kujikimu kimaisha? Leo tunazindua kampeni ambayo tutazawadia pesa taslimu na tunaamini hizi pesa zitainua maisha ya wateja wetu,” aliongeza Bw. Steve Gannon.
Uzinduzi wa promosheni hii pia ulihudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu (Group Managing Director) Bw. Charles Ireland na Mkurugenzi Mkuu wa Masoko na Ubunifu (Group Marketing and Innovation Director) Ms. Debra Mallowah. Wengine waliohudhuria ni Maofisa kutoka bodi ya Bahati Nasibu, maofisa wa PWC na Push Mobile. Pia walihudhuria washindi waliowahi kushinda zawadi mbalimbali katika promosheni za nyuma.
Kwa upande wake, Rahma Ali aliyeshinda Pikipiki shindano lililopita alisema ameongeza kipato chake kwa kukodisha pikipki yake kutumika kwa usafiriwa wa ‘bodaboda’. Kazi ambayo na Richard Mbezi ambaye alijishindia Bajaj shindano lililopita alikiri kwamba amenufaika na ushindi huo kwani kwa sasa bajaji yake inakodishwa inampatia kipato na pia ametoa ajira kwa mtu mmoja.