Watanzaia Wautingisha Mji wa Koloni Ujerumani!

wasanii wa kikundi cha Wabantu group wakiipeperusha TZ


Chereko ! Chereko za Sherehe za miaka 49 ya muungano wa Tanzania !

Siku ya Jumamosi 27.04.2013 Watanzania Wanaoishi Ujerumani , chini ya mwamvuli wa umoja wao (UTU) Waliuhakikishia ulimwengu kuwa neno “MUUNGANO” lina maana
kamili kwa maisha ya  mtanzania na binadamu wengine.

Ali Siwa wa Ubalozi wa TZ Berlin,akizungumza na Mzee.Katabalo (mtumishi mstaafu wa UN)


Sherehe hizo zilizowakusanya watanzania na marafiki wa Tazania kutoka kila kona  ya ujerumani, ziliutingisha mji wa koloni katika Usiku usio kwisha wa kusherehekea miaka 49 ya muungano wa Tanzania.

Mhe.Ali Siwa naibu balozi wa Tanzania nchini Ujerumani alikua mstari wa mbele akiwaongoza watanzania katika Muungano Day,

Nashe Mvungi akionyesha bidhaa za Tanzania kwa wageni

Wasanii mbali mbali walitumbuiza jukwaani na kuipeperusha vilivyo bendera ya Tazania.
Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania ujerumani Mh.Mfundo na kamati yake wameahidi
kufanya mambo makubwa na kuitangaza  Tanzania kwa hali na mali chini  ya  Umoja wa watanzania Ujerumani(UTU)

Ali Siwa,mwakilishi wa Ubalozi wa Tanzania,Berlin akitoa hotuba ya Ufunguzi,