Wanajeshi Kutoka Nigeria Waitembelea Wizara ya Habari

Wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria wakiwa katika picha ya pamoja  na wafanyakazi wa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati walipoitembelea wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam. Wanajeshi hao  kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu wako nchini kwa  ziara ya mafunzo ya siku tano.

Katibu Mkuu wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda  (kulia) akiangalia picha ya nembo ya chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria aliyopewa na Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali  Ati John (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya wanajeshi 22 kutoka chuo hicho wako nchini kwa  ziara ya mafunzo ya siku tano.

Kanali Anderson Msuya (kushoto) kutoka Jeshi la Wananchi la wa Tanzania (JWTZ)  akiongea jambo na Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali  Ati John wakati wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu walipoitembelea wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Mchezo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Bodi ya Filamu na Michezo ya kuigiza Joyce Fisoo akielezea kuhusu kazi za bodi hiyo kwa wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria walipoitembelea wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Joyce Hagu ambaye ni Kaimu Mkurugenzi msaidizi Idara ya utamaduni.

Picha na Anna Nkinda – Maelezo.