Shibuda aigeuka chadema, aomba posho zibadilishwe jina

Mbunge John Shibuda

Dodoma

MBUNGE wa Maswa Magharibi John Shibuda (Chadema) amewaugeuka wabunge wa chama hicho kwa kuitaka Serikali kuongeza posho za wabunge badala ya kuziondoa.

Amesema kuwa kwa majukumu ambayo yanafanywa na wabunge hasa wa aina yake ambaye ni mbunge kwa ajili ya maslahi ya jamii na si binafsi ni vema posho zikaendelea kutolewa na kutaka ziitwe malipo ya mwia.

Shibuda alitoa kauli hiyo jana mjini hapa wakati akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambapo alisema ni bora akawa mkweli na wakatofautiana kifikra lakini
awakawa amesema kile ambacho anakiamini.

Alisema alisema kuwa kwa mbunge ambaye anashiki katika misiba, anachangia shererehe, anachangia mambo ya jamii na kushirikiana kikamilifu na wananchi atakuwa anahitaji fedha hizo za posho anazoziita ujira wa mwia.

“Naomba Serikali ihakikishe inalipa mwai hizi za wabunge kwa haraka, tena ikwezekana iwe hata laki tano, najua wapo ambao wanaweza kunitafsiri vibaya lakini nachoweza kusema kwa wale ambao wananipenda wataninatafsiri vizurina wasionipenda watanitafsiri vibaya.

“Tunahitaji kupea fedha hizi kwasababu tunataka kuwatumikia wananchi wetu kikamilifu. Hawa wabunge ambao wanafanya kazi kwa ajili ya maslahi binafsi watakuwa na mitazamo yao,” alisema Shibuda na kuongeza kuwa lazima ujiwa wa Mwia uongezwe kwa wabunge.

Kutokana na kauli hiyo ya Shibuda ni wazi amewageuwa wabunge wa CHADEMA ambao walikuwa wametoa msimamo kuwa wamekubaliana kuwa wapo tayari kukata posho hizo lakini kitendo cha Shibuda kuja na msimamo tofauti wakata posho hizo ziendelee kulipwa.

Shibda katika kuzungumzioa hilo alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha wabunge wanaendelea kupewa haki zao kwa maslahi ya kuendelea kuwatumikia wananchi kwa fedha ambazo wanazipata kutokana na majukumu yao ya kuwatumikia wananchi.

Pia alisema kuwa hataopenda kuona Chama Cha Mapinduzi (CCM) inakiufa lakini anataka kuona wanajirekebisha kwa kuondoa ufisadi uliopo ndani ya chama hicho na kwa watumishi wa Serikali na kuongeza kujivua gamba haitoshi.

Alisema kuwa umefika wakati kwa Serikali kuhakikisha inaondokana na ufisadi lakini akatumia nafasi hiyo kusema amejifunza mambo mengi kwenye siasa hasa kutokana na kuwa ndani ya chama tawala na sasa amejiunga na upinzani lakini
kibaya zaidi ukiwa upinzani unaonekana si mwenzao.

Alisema kwa mazingira ambayo yanafanywa na watumishi wa umma kwa wapinzani yanasikitisha lakini akatumia nafasi hiyo ufike wakati wa kuondokana na dhana ya kuwachukia wapinzani.